Yiomyokea khalid Ibn al walid katika vita vya Muta
Khalid Ibn al walid kwa mara ya kwanza akiwa Muislamu alishiriki vita vya Muuta. Hivi ni vita vilivyopiganwa kati ya waislamu na watu wa Peshia wakichanganyika na Sasanid mwaka 629 mwezi wa 9 katika kijiji kilichoitwa Mu'ta
Sababu ya vita vya muuta ni kulipiza kisasi cha muislamu aliyeuliwa wakati akitekeleza majukumu aliyopewa na Mtume Muhammad. Mtume Muhammad (s.a.w) alimtuma Al-Harith bin Umair Al-Azdi (R.A.) kwenda Basra kupeleka barua ya kuwalingania katika dini ya Uislamu. Lakini akiwa njiani alikamatwa na Shurahbil bin Amrul-Ghassani ambaye ni gavana wa Balqa. Katika wakati huo kumuuwa mjumbe ni katika makosa makubwa na ni sawa na kutangaza vita.
Jeshi la waislamu lilikuwa na askari 3000 huku jeshi la makafiriblikawa na idadi kubwa sana ya askari. Baadhi ya wanahistoria wa kiislamu wametaja kuwa makafiri walikuwa na jeshibkatibya askati 100000 hadi 200000. Hata hivyo wanahistiria wa leo wanataja kuwa wanajeshi wa kikristo walikuwa 10000 ama chini ya hapo.
Makamanda wa kikosi cha waislamu walikuwa ni Zayd ibn Haritha, Ja'far ibn Abi Talib, na Abd Allah ibn Rawahah na wote walikufa vitani. Makamanda hawq walichaguliwa na Mtume mwenyewe. Pia aliwapangilia kwa myiririko kuwa atanza Zayd akifa atachukuwa uongozi Ja'far na akifa atachukuwa Ibn Rawah.
Makamanda walipigana kiume hadi wote wakauwawa kwa mpangilio huo huo. Baada ya kuuliwa makamanda wote jeshi la waislamu lilipata mtafaruku na hapo Thabit ibn Aqram akachukuwq bendera kuwa kama kiongozi.
Baada ya hapo akampatia uongizi khalid Ibn al walid. Sasa Khalid kwa mara ya kwanza anapewa kazi ya kuongoza jeshi la waislamu. Baada ya kuoigana kiume khalid akagunduwa kuwa waislamu wamezidiwa na hivyo watafute njia ya murudi nyumbani salama.
Khalid alilipanga vyema jeshi lake katika muonekano kuwa wataonekana kama nj wageni. Yaani kumfanya adui ahisi kama jeshi la waislamu limeongezeka. Hivyo akawapanga katika swafu tifauti na walivyokuwa siku chache zilizopita. Mfano waliokuwa wanapigana uoande wa kulia wapelekwe nyuma kushito na wanyuma kushito wapelekwe mbele kulia.
Basi makafiri wqlivyoona vile wakapata mshangao na kuhisi kuwa wenzetu wamepata nguvu mpya. Khalid alipoona makafiri wamepata woga ndipo akaamrisha jeshi lishambukie kwa nguvu zote na japo makafiri wakapata mvurugiko kwenye safu zao na wengi waliuliwa hapo.
Khalid akatumia mvurugiko huo na kuanza kurudi nyuma kidogo kidogo. Huku makafiri wqkiogopa kuwafatilia wakidhani wanaweza kuzungukwa. Hatimaye khalid aliweza kulirudisha jeshi la Waislamu salama.
Waislamu 12 tu waliweza walikufa mashahidi. Makafiri waliokufa kwenye vita idadi yao haijulikani, ijapokuwa inasemekana ni kubwa sana. Hata hivyo baadhi ya nukuu zinasema idadi yao ni kubwa kuliko idadi ya waliokufa katika waislamu. Wanahistoria wa leo wanakataa kuhusu idadi ya walokufa katiika jeshi la waislamu kuwa ni ndogo ukilinganisha na wingi wa jeshi la adui pamoja na njia iliyotumika kupigana. Hata hivyo bado hakuna ushahidi wa kuthibitisha idadi wanayoikubali.
Kwa maelezo zaidi ya vita hivi tafadhali rejea makala yetu ya vita vya Muta
https://www.bongoclass.com/madrasa/historia-ya-vita-vya-muta
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1510
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Nasaha za Lut(a.s) kwa Watu Wake
Nabii Lut(a. Soma Zaidi...
Historia ya Vijana wa Pangoni
Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s. Soma Zaidi...
NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...
Je, Nabii Isa(a.s) ni Mtoto wa Mungu?
Mwenyezi Mungu si kiumbe. Soma Zaidi...
Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...
Ijuwe Dua ya Ayyuub(a.s)
Nabii Ayyuub(a. Soma Zaidi...
NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA) BINTI KHUWALD
MTUME Muhammad (s. Soma Zaidi...
Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume
Soma Zaidi...
Yusufu(a.s) Atupwa afungwa Gerezani
Mkewe Al-Aziz hakumkatia tamaa Yusufu(a. Soma Zaidi...
Sababu za makafiri wa kiqureish kuupinga ujumbe wa uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kuhifadhiwa kwa Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Mfumo wa ulinzi na usalama katika fola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...