image

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.


Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.a.w). Makafiri hao walichimba mahandaki na ndani yake wakawasha moto mkubwa kisha wakawa wanawatosa waumini humo mmoja baada ya mwingine. Dhun-Nuwas mmoja



wa waliokuwa wafalme wa Mayahudi; aliingia Najran akiwa na jeshi kubwa ili awalazimishe watu wa Najran wasifuate mafundisho ya Mitume. Watu wa Najran walipokataa kumfuata, alichimba handaki kubwa akawasha moto akawa anamtumbukiza Muumini mmoja baada ya mwingine huku yeye na watu wake wanachekelea. Habari hii inaelezwa katika Suratul-Buruj, kama ifuatavyo:




“(Kuwa) wameangamizwa watu waliowaadhibu Waislamu katika mahandaki. Yenye moto wenye kuni (nyingi). Walipokuwa wamekaa hapo (Waliangamizwa makafiri hao pale wakati walipokuwa) wanatazama yale wanayowafanyia hao Waislamu (walipokuwa wakiwaadhibu). Nao hawajaona baya lolote kwao (Waislamu) ila kumuamini Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda (na) Mwenye kusifiwa. Ambaye ni Mwenye Ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona kila kitu” (85:4-9).



Kisa hiki kimesimuliwa kiwape fundisho na kuwaliwaza waumini wa zama zote; kwamba taabu iwapatayo kutoka kwa makafiri imeanza kuwafikia ndugu zao waliotangulia. Aidha, kutokana na kisa hiki Waislamu wanapata funzo kuwa kubakia na Imani Thabiti na suala la kusimamisha Uislamu katika jamii, kwahitaji juhudi na subira kubwa sana.

Mwenyezi Mungu anawaliwaza Waislamu kuwa makafiri wanaowatesa na kuwaghasi Waislamu hivi leo, atawaadhibu na kuwatesa kweli kweli kama alivyowatesa As-habul- Khudud.




“Hakika wale waliowaadhibu Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, kisha wasitubie basi watapata adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu ya kuungua (barabara)” (85:10). “Hakika kutesa kwa Mola wako ni kukali (sana)” (85:12).



Lakini pamoja na kuliwazwa huko; Waislamu hawatakiwi walale usingizi wasubiri nusura ya Mwenyezi Mungu. Ni wajibu wao wajiandae kwa kila mbinu kupambana na vitimvi vya maadui zao.



“Basi waandalieni (wawekeeni tayari) nguvu mziwezao (silaha), mafarasi yaliyofungwa tayari tayari ili kwazo muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu .................” (8:60).



                   



           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 253


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII ADAM
Soma Zaidi...

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija
Baada ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Mateso waliyoyapata waislamu wa mwanzo Maka, na orodha ya waislamu walioteswa vikali
Pili, Maquraish walimuendea Mtume(s. Soma Zaidi...

Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba
Mtume (s. Soma Zaidi...

Mchango wa Waislamu Katika Kuleta Uhuru Tanganyika
i. Soma Zaidi...

Nabii Isa(a.s) Azungumza Akiwa Mtoto Mchanga
Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba. Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA MTUME IDRISA (A.S)
Mtume aliyemfuatia Nabii Adam(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MAISHA YA MTUME S.A.W KABLA YA UTUME
MAISHA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na maandalizi haya ya ki ilhamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Isa(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa mahakama na mahakama ya Kadhi wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...

Wapinzani wa Ujumbe wa Nabii Salih(a.s)
Baada ya Nabii Salih(a. Soma Zaidi...