image

Maandalizi ya Hijra ya Mtume na Mafunzo tunayoyapata kutoka katika hijra hii

Maandalizi ya Hijra ya Mtume (s.

Maandalizi ya Hijra ya Mtume na Mafunzo tunayoyapata kutoka katika hijra hii

Maandalizi ya Hijra ya Mtume na Mafunzo tunayoyapata kutoka katika hijra hii

Maandalizi ya Hijra ya Mtume (s.a.w) na Waislamu kuhamia Madinah.
Mtume (s.a.w) hakuhama mpaka alipoletewa amri ya kuhama, na aliindaa safari yake kistretejia akiwa sahibu wake Abubakar (r.a).



Mikakati na Maandalizi ya Kistretejia aliyofanya Mtume (s.a.w) na Abubakar (r.a) kabla ya kuanza safari ya kuhama kwenda Yathrib (Madina);



i.Walipanga kuwa watajificha katika pango Thaur kwa siku tatu kabla ya kuanza safari ya kuelekea Yathrib (Madinah).



ii.Walipanga kutumia njia ya uficho isijulikana na mtu ya kuelekea kusini badala ya njia ya kawaida ya kuelekea kaskazini.



iii.Walimkodi bedui mweledi wa njia ile atakayewaongoza mpaka Yathrib kwa dinari 300.



iv.Abubakar (r.a) alinunua ngamia wawili kwa ajili ya safari yake na Mtume (s.a.w).



v.Abubakar (r.a) alimchukua bint yake Asma kwa siri ili kumuonyesha pango lilipo na awe anawaletea chakula muda watakapo kuwa pangoni.



vi.Pia Abubakar (r.a) alimwagiza mchunga mbuzi wake awe anachungia karibu na pango ili awapatie maziwa.



vii.Abubakar (r.a) pia alimpa jukumu kijana wake Abdullah kuwaletea taarifa za mjini kwa yatakayojitokeza baada ya wao kuondoka.



Maquraish baada ya kubaini kuwa waislamu wameshahamia Yathrib, na Mtume (s.a.w) anajiandaa naye ahame, walipanga njama ya kumuua kabla hajahama.



Maquraish walichagua vijana shupavu kutoka kila ukoo wa kiquraish na kuwapa mapanga makali ili wajewamvamie kwake akiwa amelala usiku kwa pamoja ili lawama ya kumuua isiangukie ukoo mmoja.



Kabla ya kuondoka, Mtume (s.a.w) alimkabidhi Ali (r.a) amana zote za watu ili kuwarejeshea na akamwamuru alale katika kitanda chake.



Allah (s.w) alimnusu na kabla ya Alfajir, Mtume (s.a.w) aliondoka pamoja na Abubakar (r.a) kuelekea pangoni akawaacha ‘wauaji’ nje ya nyumba yake wamelala fofofo.



Kufeli kwa zoezi la kumuua Mtume (s.a.w), Maquraish walitangaza zawadi ya ngamia 100 kwa atakaye mleta Muhammad au Abubakar yuko hai au amekufa.



Maquraish kwa kumkodi bedui mjuzi wa kufuatilia nyayo, akiwaongoza mpaka pangoni lakini Allah (s.w) aliwanusu. Rejea Qur’an (9:40).



Mwishowe baada ya siku tatu, Mtume (s.a.w) na sahibu wake, Abubakar (r.a) waliondoka kuelekea Madinah na walifika salama kabisa.



Kwa heshima ya Mtume (s.a.w), mji wa Madinah ukawa unaitwa ‘Madinatul-Munwwarah’ (mji ung’aao).



Baada ya kufariki (kutawafu) Mtume (s.a.w), Waislamu walikubaliana kuanzisha Kalenda ya mwaka wa Kiislamu ‘Al-Hijrah’ (A.H) ianzie siku ile aliyohama (hijra ya) Mtume (s.a.w) kwenda Madinah.



Mafunzo yatokanayo na Hijrah ya Mtume (s.a.w) na Maswahaba wake.
i.Hatuna budi kutunza na kurejesha amana za watu kwa wenyewe bila kujali uadui wao kwetu.



ii.Waislamu hawanabudi kuweka mipango na mikakati madhubuti juu ya namna ya kutekeleza mambo yao kabla ya utekelezaji wake.



iii.Waislamu hawana budi kuchukua tahadhari katika kuendesha harakati za kidini kwa kuzingatia kuwa dini ya Uislamu ina maadui wengi.



iv.Nusura ya Allah (s.w) na Ushindi hupatikana tu baada ya kufanyika jitihada za dhati katika kuusimamisha Uislamu katika jamii na kumtegemea yeye pia.



v.Waislamu wanalazimika kufanya jitihada ya dhati ya kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo kwa kila kipengele cha maisha yao, kama mazingira yatakuwa ndio kikwazo hawanabudi kuhama (kuhajiri) kwenda sehemu (ardhi) yenye wasaa.
Rejea Qur’an (4:97-99).



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 468


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)
Mtume(s. Soma Zaidi...

Kuandaliwa kwa Muhammad kabla ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA MAMA AMINA MKE WA ABDALLAH MTOTO WA ABDUL-AL MUTALIB
KUZALIWA KWA MTUME (S. Soma Zaidi...

HISTORIA YA WATU WEMA WALIOTAJWA KWENYE QURAN
Soma Zaidi...

Imam Abu Hanifa: Nuuman Ibn Thabit
Soma Zaidi...

Kuandaliwa Mtume(s.a.w) maandalizi ya kimafunzo na maandalizi ya ki ilham
Mitume huzaliwa Mitume. Soma Zaidi...

Kuangamia kwa Mtoto na Mke wa Nuhu(a.s)
Tukirejea Qur’an (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a. Soma Zaidi...

Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah
Baada ya mikataba miwili ya ‘Aqabah na baada ya Waislamu 75 kufika Yathrib salama, Mtume(s. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Nuhu(a.s)
(i) Tuanze kulingania kwa Tawhiid – kumjua Allah(s. Soma Zaidi...

Kuhifadhiwa kwa Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nabii Isa(a.s) Azungumza Akiwa Mtoto Mchanga
Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba. Soma Zaidi...

Vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kif cha khalifa Uthman
Soma Zaidi...