HISTORIA YA NABII SHU’AYB(A.S)
Nabii Shu’ayb(a.
HISTORIA YA NABII SHU’AYB(A.S)
Nabii Shu’ayb(a.s) alitumwa kwa watu wa Madian waliokuwa wakikaa pande za pwani ya Shamu (Syria). Watu hawa walikuwa wafanyabiashara wakubwa wa zama hizo. Mji wao ulikuwa katika njia kuu (Highway) ya misafara ya biashara kutoka sehemu mbali mbali za Mashariki ya kati kuelekea pwani ya bahari ya Mediterranean.
Tabia ya watu wa Madian
Wamadian pamoja na kuwa wafanyabiashara mashuhuri walikuwa na tabia ya kupunja vipimo wakati wa kuuza. Pia walikuwa wababe wakifanya uharibifu katika ardhi, walikuwa majambazi wakipora na kunyang’anya watu mali zao. Vile vile walikuwa washirikina na kuzuia watu kufuata Dini ya Allah(s.w).
Ujumbe wa Nabii Shu’ayb kwa Watu Wake
Nabii Shu’ayb(a.s) kama walivyofanya Mitume waliomtangulia aliwanasihi watu wake kumwamini na kumuabudu Allah(s.w) ipasavyo katika maisha yao ya kila siku na kusimamisha uadilifu katika jamii.
Na kwa watu wa Madian (tulimpeleka) ndugu yao, Shuaibu. Akasema: “Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Msipunguze kipimo (cha vibaba) wala (cha) mizani. Mimi nakuoneni mumo katika hali njema (basi msiiharibu kwa kufanya dhulma).Nami nakukhofieni adhabu ya siku (kubwa) hiyo itakayokuzungukeni.” (11:84)
Nabii Shu’ayb(a.s) aliendelea kuwaasa watu wake:
“Wala msikae katika kila njia kuogopesha (watu) na kuwazuilia na Dini ya Mwenyezi Mungu (wale) wenye kuamini, na kutaka kuipotosha Na kumbukeni mlipokuwa wachache, Naye akakufanyeni kuwa wengi (sasa).Na tazamneni jinsi ulivyokuwa mwisho wa waharibifu.” (7:86)HISTORIA YA NABII
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 ai web app 👉4 web hosting 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...Kisa cha Israa na Miraji na kufaradhishwa swala tano
Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B.
Soma Zaidi...Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake
Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s.
Soma Zaidi...Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.
Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.
Soma Zaidi...Kujengwa upya al Kabah baada ya kuwa na mipasuko.
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 18. Hapa utajifunza kuhusu tukio la kujengwa upya kwa al kaaba 🕋
Soma Zaidi...