image

Khalifa na Utungaji Sheria, na utiifu juu ya sheria na usimamiaji wa haki

Khalifa na Utungaji Sheria, na utiifu juu ya sheria na usimamiaji wa haki

Khalifa na Utungaji Sheria



Khalifa kama ilivyokwishaoneshwa sio mtungaji wa sheria kama ilivyo kwa marais wa leo na mabunge yao. Khalifa ni mtekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu na msimamizi mkuu wa sheria za Mwenyezi Mungu. Katika kipindi cha Ukhalifa vyanzo vya sheria vilibakia kuwa Qur’an, Sunnah na Ijmaa na baadaye Umar, Khalifa wa pili, aliongeza Qiyas. Kwa hali hii Ufalme katika Dola ya Kiislamu ulibaki kuwa ni wa Mwenyezi Mungu tu.


Siku za mwanzo za ukhalifa kuliundwa tume ya sheria (Ofisi ya Mufti) ilipotokea haja. tume hii iliitwa na kupitisha uamuzi. Tume ya sheria ya Khalifa ilifanya kazi kwa kutegemea vyanzo vya sheria vilivyotajwa katika masuala ya kawaida, maamuzi ya tume yalikidhi haja. Lakini yalipotokea masuala yasiyo ya kawaida na yenye umuhimu wa kitaifa ilikaa majlis ya Answar, Muhajirin, wawakilishi wa Aus na Khazraj na kupitisha maamuzi; kwa mfano baada ya kutekwa kwa Iraq na Syria wapo maswahaba waliotaka ardhi igawiwe kwa askari waliopigana. Majlis iliyojumuisha Ansar, Muhajirin na watu mashuhuri watano watano kutoka makabila ya Aus na Khazraj ilifanyika kuamua suala hili.


Baada ya mjadala mrefu Khalifa Umar alifanikiwa kuwaelewesha wajumbe wa majlis kwa kunukuu aya nyingi kuthibitisha kuwa katika ardhi hata vizazi vijavyo vina hisa kwa hiyo ardhi isigawiwe kwa askari waliopigana lakini waachiwe wenyewe waliotekwa na kodi itakayotokana na ardhi hii wagawiwe askari katika mfumo wa kiinua mgongo cha kila mwaka.


Hivyo ni dhahiri mkono wa Khalifa haukuwa juu ya sheria bali chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu, kwa namna hii haikuwezekana kupendelea kundi au mtu yeyote au kuipinda sheria kwa kumpendelea kundi fulani. Hivyo kulikuwa na usawa kamili mbele ya sheria. Hali kadhalika katika masuala ya kodi kulikuwepo usawa na haki za kiraia. Hali hii ilipelekea mshikamano miongoni mwa waumini, uhuru wa maoni, haki katika jamii na kubwa kabisa ni kuwavumilia wafuasi wa dini nyingine.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 223


Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰2 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kiafrika hapo zamani
3. Soma Zaidi...

Kukomeshwa kwa Riddah na Chokochoko Nyingine katika dola ya kiislamu
Soma Zaidi...

Historia ya Firaun, Qarun na Hamana
Karun na Hamana waliishi zama za Mtume Musa(a. Soma Zaidi...

Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Soma Zaidi...

Imam Nasai na kitabu cha Sunan
Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Bani Israil
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII ISA
Soma Zaidi...

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina
Soma Zaidi...

Imam Bukhari na Sahihul Bukhari
Soma Zaidi...

Vita vya Al Fijar na sababu zake
Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Hud(a.s)
(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s. Soma Zaidi...

Historia ya Vijana wa Pangoni
Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s. Soma Zaidi...