Katika kuwafikishia ujumbe watu wake,Nabii Shu’ayb alifanya yafuatayo:
Kwanza, kuwafahamisha watu wake kwa uwazi kuwa yeye ni
Mtume wa Allah(s.w) aliye mfano wa kuigwa:
Akasema: “Enyi watu wangu! Mnaonaje kama ninayo dalili inayotokana na Mola wangu na ameniruzuku riziki njema (ya Utume) kutoka kwake (nitaacha haya, nishike upotofu wenu)? Wala sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayokukatazeni. Sitaki ila kutengeneza, kiasi ninavyoweza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu (Mwenyewe). Kwake ninategemea, na Kwake naelekea.” (11:88)
Pili, aliwahofisha adhabu kali ya Allah(s.w) iwapo watakataa kumwamini na kumfuata.
Na kwa Madiani (tulimtuma) ndugu yao, (Nabii) Shu’ayb, naye akasema: “Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu na iogopeni siku ya akhera wala msende katika ardhi mkifisidi.” (29:36)
Tatu,aliwatahadharisha watu wake na adhabu ya Allah(s.w)
iliyowafika kaumu zilizopita za akina ‘Ad, Thamud na kaumu Lut.
“Na enyi watu wangu! Kukhalifiana nami kusikupelekeeni yakakusibuni kama yaliyowasibu watu wa Nuh au watu wa Saleh na watu wa Luti si mbali nanyi.” (Karibuni hivi wameangamizwa; na nchi zao ziko karibu na nyinyi pia). (11:89)
Nne, aliwatumainisha watu wa Madian kuwa endapo wataomba msamaha kwa Allah(s.w) na kutubu juu ya makosa yao, Allah(s.w) atawasamehe na kuwaepusha na balaa lililowafika watu wa kaumu za Mitume waliotangulia.
“Na ombeni msamaha kwa Mola wenu (kwa yaliyopita), kisha tubuni kwake . Hakika Mola wangu ni Mwenye kurehemu na Mwenye kuwapenda (waja Wake).” (11:90)
Tano, aliwaonyesha msimamo na utegemezi wake juu ya
Allah(s.w).
“Na enyi watu wangu! Fanyeni (mtakayo) kwa tamkini yenu; na mimi pia ninafanya (yangu kwa tamkini yangu). Karibuni hivi mtajua ni nani itakayemfikia adhabu ifedheheshayo na ni nani aliye muongo. Na ngojeeni; mimi pia ninangoja pamoja nanyi.” (11:93)
“Bila shaka tumemtungia Mwenyezi Mungu uwongo ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Mwenyezi Mungu kutuokoa nayo. Wala haiwi kwetu sisi kurejea mila hiyo. Lakini akitaka (jambo) Mwenyezi Mungu, Mola wetu, (huwa). Mola wetu amekienea kila kitu kwa ilimu yake. Kwa Mwenyezi Mungu tunategemea. Mola wetu! Hukumu baina yetu na baina ya wenzetu (hawa) kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanaohukumu.” (7:89)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Katika kufikisha ujumbe huu kwa watu wake Nuhu(a.
Soma Zaidi...Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a.
Soma Zaidi...Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.
Soma Zaidi...Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a.
Soma Zaidi...