Mtume Yusufu(a.
Mtume Yusufu(a.s) alikuwa mtoto wa Mtume Ya’aquub bin Is- haq bin Ibrahiim. Kwa hiyo Yusufu(a.s) ni kijukuu cha (mjukuu wa mtoto wa) Mtume Ibrahiim(a.s) na mjukuu wa Mtume Is-haqa(a.s.).
Mtume Ya’aquub(a.s) alikuwa na watoto 12. Nabii Yusufu(a.s) alichangia mama na mmoja wa hao. Wengine 10 walikuwa na mama zao.
Ndoto ya Nabii Yusufu(a.s) Maisha ya Nabii Yusufu(a.s) yanaanza kusimuliwa ndani ya Qur’an pale alipomwambia babake kuwa:
Yusufu alipomwambia baba yake “Ewe babaangu! hakika nimeona katika ndoto nyota kumi na moja na jua na mwezi. Nimeviona hivi vikinisujudia(12:4)
Mtume Ya‘aquub, kwa ilimu aliyopewa na Mola wake alifahamu tafsiri ya ndoto ile kwamba inabashiri kuwa Yusufu atakuja kuwa mtu mwenye hadhi kubwa na Mtume. Akamtahadharisha kuwa:
Akasema (baba yake): “Ewe mwanangu! Usiwasimulie ndoto yako (hii) nduguzo wasije wakakufanyia vitimbi (kwa ajili ya husuda). Hakika Shetani kwa mwanadamu ni adui aliye dhahiri.(12:5)
Namna hivi Mola wako atakuchagua na kukufundisha hakika ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya kizazi cha Ya‘aquub, kama alivyoitimiza zamani juu ya baba zako Ibrahim na Is-haqa. Bila shaka Mola wako ni Mjuzi na Mwenye hikima: (12:6).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Pamoja na Ucha-Mungu aliokuwa nao Nabii Sulaiman watu hawakuacha kumsingizia mambo machafu.
Soma Zaidi...Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara.
Soma Zaidi...Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.
Soma Zaidi...Pamoja na upinzani mkali alioupata kutoka kwa viongozi wa makafiri, Nabii Nuhu(a.
Soma Zaidi...