Vitimbi vya Wapinzani Dhidi ya Ujumbe wa Nabii Shu’ayb(a.s)

Kama ilivyokuwa katika kaumu zilizotangulia, waliomuamini Shu’ayb(a.s) na kufuata nasaha zake walikuwa watu wachache tu katika jamii yake. Wengi wao walikaidi mafundisho ya Mtume wao wakiongozwa na wakuu wa jamii. Katika kumkanusha Mtume wao walitumia mbinu mbali mbali.



Kwanza, walitumia vitisho
Wakuu waliotakabari katika kaumu yake wakasema: “Ewe Shu’ayb! Tutakutoa wewe na wale walioamini pamoja nawe katika mji wetu, au mrejee katika mila yetu.” Akasema: “Je, ingawa tunaichukia?” (7:88)



Pili, walitumia mbinu ya kuwakatisha watu tamaa

Na wakuu waliokufuru katika kaumu yake wakasema: “Kama nyinyi mkimfuata Shu’ayb, hapo bila shaka mtakuwa wenye kukhasirika.” (7:90)



Tatu,walimdhihaki Mtume wao.

Wakasema: Ewe Shuaibu! Swala zako zinakuamrisha tuyaache yaliyokuwa wakiyaabudu baba zetu au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Bila shaka wewe ni mwenye akili na mnyoofu (11:87)



Nne, walitumia mbinu ya kumdhalilisha.

Wakasema: “Ewe Shu’ayb! Hatufahamu mengi katika hayo unayoyasema. Na sisi tunakuona mdhalilifu kwetu. Lau kuwa si jamaa zako tungekupiga mawe, wala wewe si mtu mtukufu kwetu! (ila tunachunga hishima ya jamaa zako tu).” (11:91)