Kuangamizwa Waovu na Kuokolewa Waumini


Baada ya kuonywa wasionyeke, Allah(s.w) aliwaangamiza kama walivyoangamizwa akina Ad, Thamud, n.k.Basi mtetemeko wa ardhi uliwatoa roho zao, wakawa wasiojimudu, (wamekufa) humo mjini mwao. Wale waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa kama kwamba hawakuwako (mahala hapo). Wale waliomkadhibisha Shu’ayb ndio waliokuwa wenye khasara. (7:91-92)Na ilipokuja amri yetu, tulimuokoa Shu’ayb na wale walioamini pamoja naye kwa rehema yetu. Na wale waliodhulumu ukelele (wa adhabu) ulinyakuwa roho zao. Wakawa majumbani mwao wametulia tu (wamekufa).(11:94)
Kama kwamba hawakuwamo humo. Sikilizeni. Wameangamia (watu wa) Madiana kama walivyoangamia (kina) Thamudu. (11:95)

Kwa mujibu wa aya hizi, watu wa Madian waliangamizwa kwa ukelele ukifuatiwa na tetemeko la ardhi. Tukikumbuka kuwa:Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu; Mwenye hikima. (48:7)