Sunnan Abu Daud

Sunnan Abu Daud ni kitabu cha Hadith cha Abu Daud. Imamu Abu Daud alizaliwa 203 A.H. na akafiriki 275 A.H. Elimu yake ya mwanzo aliipata Khurasan. Alisafiri sehemu mbali mbali ambazo zilikuwa mashuhuri kwa kuwa na wanazuoni wa Hadith. Ni miongoni mwa wanafunzi wa Imam Ahmad bin Hambali. Alikusanya Hadith 500,000 na alizoziandika katika kitabu chake cha Hadith kinachojulikana kwa jina la "Sunnan" ni Hadith 48,000 tu.

Japo hakuwa mkali sana katika uchambuzi na uhakiki wa Hadith zake kama walivyokuwa Bukhari na Muslim, Sunan yake imekuwa ni kitabu cha Hadith mashuhuri sana kwa Umma wa Kiislamu na imeshika daraja la 2 kwa usahihi baada ya sahihi mbili. Hapana shaka kitabu hiki kimejaza mapengo ya mambo yale ambayo hayakugusiwa na Imam Bukhari na Imamu Muslim. Pia Abu Dawud naye alipanga Hadith zake kulingana na vichwa vya habari vya mada mbali mbali.