Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a.
Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a.s) alipata majaribu mengi katika harakati za kuhuisha Uislamu alipokuwa nchini mwake Iraq. Baba yake alimfukuza nyumbani na jamii nzima ikamtenga na kumuhukumu kuchomwa moto hadharani. Bila shaka alipata madhila ya aina hiyo hiyo alipokuwa amewalingania Uislamu washirikina wa nchi nyingine alimohamia. Kama hiyo haitoshi Allah(s.w) alimuongezea mingine miwili mizito.
Mtihani wa kwanza, ni pale alipoamrishwa na Mola wake, kujitenga na mkewe Hajira na mtoto wake mchanga, Ismail, na kuwaacha peke yao jangwani karibu na Ka’abah. Nabii Ibrahiim(a.s) alitii amri hii ya Mola wake na kutegemea msaada wake kwa familia yake huku akiomba dua ifuatayo:
“Mola wetu! Hakika mimi nimewaweka (nimewakalisha baadhi kizazi changu (mwanangu Ismaili na mama yake, Hajrah) katika bonde (hili la Makka) lisilokuwa na mimea yoyote; katika nyumba yako takatifu (Al- Kaaba )Mola wetu! Wajaalie wasimamishe Sala. Na ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao (wapende kuja kukaa hapa ili pawe mji) na uwaruzuku matunda ili wapate kushukuru.” “Mola wetu! Hakika wewe unajua tunayoyaficha na tunayoyadhihirisha. Na hakuna chochote kinachofichikana kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika mbingu.” (14:37-38)
Mtihani wa pili na mzito zaidi ni pale Nabii Ibrahiim(a.s) alipoamrishwa na Allah(s.w) kuwa amchinje Ismail, mtoto wake mmoja pekee, aliyekuwa anamtarajia, amsaidie katika harakati za kusimamisha Uislamu. Vile vile katika hili Nabii Ibrahiim hakusita, bali alitii amri ya Mola wake na kulitekeleza kwa moyo mkunjufu. Pia mtoto wake Ismail, alikuwa radhi kwa hili kwa ajili ya kutafuta radhi za Mola wao.
“Basi (Ismail) alipofikia (makamu ya) kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ee Mwanangu! Hakika nimeona katika ndoto ya kwamba ninakuchinja. (Na ndoto za Mitume ni wahay). Basi fikiri, waonaje?” Akasema: Ee baba yangu! Fanya unavyoamrishwa utanikuta Insha-Allah miongoni mwa wanaosubiri.” (37:102)
Basi wote wawili walipojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu), na akamlaza kifudifudi (amchinje). Pale pale tulimwita: “Ewe Ibrahimu:” “Umekwishasadikisha ndoto. (Usimchinje mwanao).” Kwa yakini hivi ndivyo tunavyowalipa watendao mema. (37:103-105)
Bila shaka (jambo) hii ni jaribio lililo dhahiri, (mtihani ulio dhahiri). Basi tukamkomboa kwa mnyama wa kuchinjwa mtukufu. (37:106-107)
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1324
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Kitabu cha Afya
Tukio la kupasuliwa kifua Mtume Muhammad S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 7 Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na mkataba wa aqabah katika kuandaa ummah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri. Soma Zaidi...
Tamko la suluhu baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...
HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...
Maswali kuhusu Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kulingania watu wake na Miujiza Aliyoonyesha Nabii Isa(a.s)
Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyewawezesha Mitume na Manabii kufanya miujiza. Soma Zaidi...
Kuanzishwa kwa dola ya kiislamu madinah
Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Historia ya vita vya Muta
hii ni historia ya vita vya Muta. Katika makala hii utajifunza sababu ya vita hivi na yaliyojiri katika uwanja wa vita. Soma Zaidi...
Historia ya uislamu wakati wa Makhalifa wanne: Abubakar, Umar, Uthman na Ally
Soma Zaidi...
Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao
Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a. Soma Zaidi...
NUHU(A.S) NA WATU WAKE NA UOVU WALIOKUWA WAKIUFANYA WATU WAKE
Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a. Soma Zaidi...