Imam Tirmidh


Imamu Tirmidh alikuwa mwanazuoni mkubwa. Pamoja na kitabu chake cha Hadith aliandika vitabu vingine vya Sharia na Tarekh. Alisafiri sana katika kukusanya Hadith katika nchi za Khurasan, Iraq na Hijaz.


Kitabu chake cha Hadith kinachojulikana kwa jina la Jami’u kimemfanya kuwa maarufu sana. Alikuwa mwanazuoni wa kwanza kuchambua Hadith kutokana na majina ya wasimulizi. Alizingatia majina yao, majina yao ya ukoo, majina ya utani, n.k. Jami'u ina Hadith chache zaidi ukilinganisha na Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim.