Mji wa Makkah na kabila la kiqureish

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

-    Mji wa Makkah ni mji mkongwe wa kihistoria ulioanzishwa na Nabii Ibrahiim miaka mingi iliyopita.

 

-    Nabii Ibrahim (a.s) na mwanae Nabii Ismail (a.s) ndio walioinua kuta za nyumba tukufu ya Ka’abah kwa amri ya Allah (s.w).

    Rejea Qur’an (2:127).

 

-    Ka’abah ni nyumba ya mwanzo na pekee ulimwenguni iliyowekwa kwa ya kuhiji wanaadamu wote ulimwenguni.

    Rejea Qur’an (22:27), (3:96) na (22:29).


 

-    Kutokana na jangwa na ukame wa mji huu, Allah (s.w) alijaalia chem.-chem ya maji ya zamzam kutokana dua ya Nabii Ibrahim (a.s).

    Rejea Qur’an (14:37).

 

-    Mji huu ulipata utukufu kutokana na uwepo wa nyumba tukufu ya Ka’aba ambapo kabila la Qureish ndio walikuwa walinzi wa nyumba hiyo.

    Rejea Qur’an (106:1-4).

 

-    Ni mji alikozaliwa Mtume Muhammad (s.a.w) mwaka 570 A.D katika kabila la Kiqureish mwaka wa ndovu.

    Rejea Qur’an (105:1-5).

 

-    Kabila la Kiqureish liliheshimika kuliko makabila mengine kwa huduma walizokuwa wakitoa kwa watu wanaohiji, misafara ya biashara na kule kuitumikia nyumba hiyo.

 

-    Kabila la Qureish ni miongoni mwa makabila ya waarabu yaliyojishughulisha sana na biashara mbali mbali ndani na nje ya Makkah kwa muda mrefu.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1498

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana: