Tamko la suluhu baada ya vita vya Siffin
Tamko la Wapatanishi
Baada ya mazungumzo marefu wapatanishi walikubaliana kuwa wote wawili Ali na Muawiyah hawafai kugombea nafasi ya ukhalifa. Amr bin al- As alimtegea Abu Mussa aanze yeye kusema msikitini juu ya maazimio yao. Abu Muusa akasema; “Enyi watu tumelizingatia vyema suala linalotukabili. Hatukuona njia nyingine ya kuleta amani miongoni mwa watu ila kuwaondoa wote katika nafasi ya kugombea Ukhalifa. Baada ya hivi mchague Khalifa anayefaa. Hii ndio hukumu yangu.
Alipopanda jukwaani Amr bin al As alibadili maneno na kusema maneno wasiyokubaliana na mwenziwe kwa kusema; “Mmesikia hukumu ya Abu Mussa. Amemuondoa mtu wake nami pia ninamuondoa. Lakini kwa chifu wangu Muawiyah, yeye ninamthibitisha, ni mrithi wa Uthman, mlipiza wa damu yake, ni bora kuliko wote kwa kuchukua nafasi yake.
Wajumbe wote walichanganyikiwa kwa kauli hii na kukawa hakuna maelewano. Nusra Amr bin al-As auliwe na askari wa Ali. Uamuzi huu haukufuata Qur’an hivyo haukukubalika. Khawarij walijikusanya na kuanza uasi. Walihama Harorah na kwenda Nahruwan. Katika eneo hili waliuwa watu na kufanya ukatili. Khalifa Ali alizungumza na Khawarij hawa ili waache vitendo vyao na imani yao potofu.
Lakini hawakukubali, kwa hali hii mapigano yakawa lazima, hata hivyo walishindwa vibaya. Baada ya hapa Khalifa Ali aliamuru jeshi lake liende Syria kupambana na Amir Muawiya kwa sababu suluhu haikuwa katika Qur’an. Lakini kabla ya kwenda Syria Khalifa Ali alipiga kambi mahali paitwapo Nakhila karibu na mji wa Kufa. Askari wake waliomba kwenda makwao na akawaruhusu, wengi hawakurudi na safari ikavunjika. Alijaribu mara mbili kukusanya askari kwenda Syria bila mafanikio na kutokana na hali hii suala zima la kupigana tena na Muawiya akaliacha.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 ai web app 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
tarekh 3
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba.
Soma Zaidi...Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.
Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi.
Soma Zaidi...Sababu ya uislamu kuwa ndiyo dini sahihi pekee
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Umuhimu wa jihad katika kusimamisha uislamu katika jamii
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...