Kuanzishwa kwa mahakama na mahakama ya Kadhi wakati wa makhalifa

Kuanzishwa kwa mahakama na mahakama ya Kadhi wakati wa makhalifa

Khalifa na Mahakama



Kabla ya kuangalia suala la mahakama katika Uislamu, tuanze na mtazamo wa Uislamu juu ya uhalifu, makosa au hatia. Makosa katika Uislamu yapo katika mafungu matatu:


(i) Makosa yanayomuhusu Mwenyezi Mungu kama vile uzinzi, ambao adhabu yake ni bakora mia moja, kumsingizia mtu kuzini, ambako adhabu yake viboko themanini, kuritadi adhabu yake ni kifo, kunywa vileo adhabu yake viboko themanini, wizi ambao adhabu yake ni kukatwa mkono na unyang’anyi au ujambazi ambao adhabu yake ni
kukatwa mkono na miguu. Makosa haya yanajumuishwa katika istilahi moja kuwa ni Al-Hudud. Khalifa hawezi kusamehe makosa haya. Kazi yake ni kutekeleza hadd (adhabu). Kwa wasio Waislamu makosa haya husameheka endapo atasilimu.


(ii) Makosa dhidi ya mwanadamu yanayohitaji fidia al-qisas.
Mengi ya makosa haya kama kuuwa, kuumiza, kumtukana mtu n.k yanaweza kumalizwa kwa makubaliano kwa mujibu wa sheria lakini Khalifa hana mamlaka ya kusamehe ila aliyekosewa. Hali kadhalika makosa haya hayahesabiwi kuwa makosa dhidi ya Serikali.


(iii) Yapo baadhi ya makosa kama, uasi (Rebellion), kula mali ya umma yamehesabika kama makosa dhidi ya Serikali.Kwa kuzingatia haya, kazi za Khalifa kimahakama ni za aina tatu. Kwanza kuhakikisha kuna amani katika himaya yake, maendeleo kwa tabaka zote za watu na kuwalinda wanyonge mbele ya wenye kujiweza. Pili ni kutekeleza adhabu, kuratibu na kutekeleza haki za wanaodhulumiwa. Na tatu ni kuteua mahakimu wa kusimamia haki.


Mahakimu hawa walikuwa watu wazima, waadilifu, waliobobea katika sheria ambao kazi zao ni pamoja na kuhukumu kesi, kusuluhisha magomvi, kurudisha amana za watu, ulipaji wa zaka, utekelezaji wa usia, utekelezaji wa adhabu, kusimamia mipango ya ndoa, mirathi, talaka, na haki za wanyonge.


Katika kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa wote, tangu wakati wa Ukhalifa wa Abubakar ilianzishwa ofisi ya mufti au taasisi ya mufti au tume ya uchambuzi wa sheria. Ofisi hii ndio pekee iliyoruhusiwa kutoa uchambuzi wa kina wa Fatwa za mamlaka mbali mbali. Hakuruhusiwa mtu mwingine kutoa uchambuzi wa sheria. Walioteuliwa wakati wa Abu bakar kushika wadhifa huu ni Umar, Ali, Uthman, Abul Rahman bin Auf, Ali bin Kaab, Zaid bin Thabit na Abu Huraira - Mufti hawa walisaidia kuwafahamisha watu kuhusu sheria na kuwashauri bila malipo. Serikali ilifanya hivi ili kupunguza makosa kwani kwa kujua sheria watu walijizuia kufanya makosa.


Waraka, Khalifa Umar,aliowatumia mahakimu ni kielelezo cha utaratibu wa mahakama ulivyokuwa wakati wa makhalifa ambao leo hii unafuatwa duniani kote. waraka huo tunaufupisha kama ifuatavyo:


(i) Utawala wa haki ni amri ya Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake, hivyo ni lazima kufuatwa.


(ii) Mashtaka yanapowasilishwa ipitishwe hukumu kwa uangalifu. (iii) Mshitaki na mshitakiwa wote watendewe haki ili maskini asikate
tamaa ya kufanyiwa haki na wenye uwezo wasifikirie kupendelewa.


(iv) Ushahidi ni juu ya mlalamikaji na anayelalamikiwa anaweza kukana anacholalamikiwa kwa kuapa.


(v) Suluhu inaweza kufikiwa nje ya mahakama lakini mazingira ya suluhu yasichupe mipaka ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu.


(vi) Hukumu inaweza kubadilishwa katika jambo lililodhahiri, kwani kubadilishwa hukumu ni bora kuliko kuendelea na uonevu.


(vii) Ikitokea kesi isiyo angukia kwenye sheria wala hukumu iliyoitangulia, ilinganishwe na kesi zinazofanana kisha deduction itumike kupitisha hukumu inayompendeza Mwenyezi Mungu na ya haki.


(viii) Mlalamikaji apewe muda wa kutolea ushahidi kesi yake ataposhindwa kesi inaweza kufutwa.


(ix) Hakimu asijione wala kuonyesha kuchukia inaposemwa kweli.


Watu wote ni sawa mbele ya sheria ndio mafunzo ya Qur’an. Uislamu hauruhusu ule msemo wa “Mfalme hakosei”. Hakuna mwanadamu aliyekamilika asiyekosea kabisa. Mtume (s.a.w.) aliweka mfano pale alipowataka watu wenye madai dhidi yake wajitokeze. Maswahaba wake nao walifuata nyayo zake kama mtu angewashitaki kama ilivyotokea kwa Umar au wao pia wangeshitaki kama ilivyotokea kwa Ali.


Khalifa umar na Ubayy ibn Kaab, walikuwa na tofauti zao. Ubayy ibn Kaab alikwenda kumshtaki Khalifa kwenye mahakama ya Zayd bin Thabit. Hivyo Khalifa aliingia mahakamani kwa kujitetea. Alipokuwa anaingia mahakamani Zayd alisimama. Hapa Khalifa alisema hili ni tendo la kwanza la kuvunja haki. Kwa kufuata nafasi ya Khalifa kuwa alikuwa anajitetea alilazimika kuapa. Hakimu Zayd alimuomba Ubayy aondoe haki yake ya kumtaka Khalifa aape. Khalifa Umar aliingilia kati na kusema “kama Umar na watu wengine siyo sawa mbele yako, hufai kuwa Hakim.33





                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1152

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Kusilimu kwa Wachawi wa Firaun

Mawaziri waliokuwa washauri wakuu wa Firauni wakataka wakusanywe magwiji waliobobea katika uchawi nchi nzima, kisha wapambanishwe na Nabii Musa(as).

Soma Zaidi...
Mfumo wa ulinzi na usalama katika fola ya uislamu madinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao

Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.

Soma Zaidi...
Si Yesu Aliyesulubiwa (yesu hakufa msalabani wala hakusulubiwa

Katika Qur,an tukufu, Mwenyezi Mungu aliye muweza na mjuzi wa mambo anathibitisha kuwa aliyesulubiwa si Nabii Isa(a.

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
tarekh 10

KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.

Soma Zaidi...
Mtume (s.a.w) alivyoandaa ummah wa kiislamu makkah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Maandalizi ya Kimafunzo aliyoandaliwa Mtume Muhammad

(i) Suratul- ‘Alaq (96:1-5)“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa ‘alaq.

Soma Zaidi...