Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)

Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a.

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)

Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a.s) tunajifunza yafuatayo


(i) Kila muumini anapotunukiwa neema na vipaji vikubwa
zaidi kuliko wengine anatakiwa amshukuru Allah(s.w) zaidi kwa kujitahidi kufanya wema zaidi na ibada maalumu za ziada kuliko watu wengine kwani hiyo ni amana na mtihani kwake. Hili aliliona Nabii Sulaiman(a.s) pale aliposema.

'.Haya ni kwa fadhila za Mola wangu, ili anijaribu nitashukuru au nitakuwa mwizi wa fadhila, na anayeshukuru anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anayekufuru kwa hakika Mola wangu ni mkwasi, karimu (27:40)- Mtume(s.a.w) katika kumshukuru Mola wake, alikuwa akisimama usiku mpaka miguuu yake ikawa inavimba. Maswahaba walipomrai kuwa asijitaabishe hivyo, kwani kashasamehewa madhambi yake yaliyopita naya baadaye, aliwajibu: 'Ni siwe mja mwenye kushukuru? '(ii) Waumini wana dhima ya kuulingania Uislamu mijini na vijijini,ufike katika kila kona ya nchi na ulimwnegu kwa ujumla tukianzia kwenye familia zetu.(iii) Kiongozi wa Harakati za Kiislamu katika jamii hanabudi kuwanamtandao wa waumini na wanaharakati watakao muwezesha kupata taarifa za hakika juu ya hali halisi ya Uislamu kutoka kila kona ya jamii husika.(iv) Nguvu za elimu, Imani thabit,uchumi na nguvu za kujeshi ni nyenzo muhimu sana katika kusimamisha uislamu katika jamii.(v) Hatunabudi kuzichunguza habari tunazozipata juu ya watu kabla ya kuzifanyia kazi- Nabii Suleiman hakumuamini Hud Hud moja kwa moja:-


'Akasema (Suleiman) Tutatazama kama unasema kweli au umo katika waongo. Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha uwaache, na utawatazama wanashauriana vipi' (27:27-28)(vi) Baada ya kupa uhakika juu ya jambo ovu,mara moja tuweke mikakati ya kuliondoa kwa kutumia mbinu zinazostahiki.(vii)Kutafuta ushauri kabla ya kufikia maamuzi ni katika sifa muhimu za kiongozi wa kiislamu.(viii)Pamoja na kutafuta ushauri kwa wadau wa jamii yake, kiongozi mweledi ni yule anayeangalia mbali. Malkia wa Sabaa pamoja na kushauriwa na mawaziri wake kuingia vitani, hakupendelea kwa kuzingatia matokeo. Aliona saluhu ni bora zaidi kuliko vita (27:34 - 35).(ix) Nikawaida ya viongozi wa kitwaghuut kuwahonga au kuwarubuni viongozi wa kiislamu kwa kuwakaribisha Ikulu, kuwapa mirunda ya pesa, magari,majumba, vyeo vya bandia n.k.(x) Kiongozi au mwanaharakati wa kiislamu anayefanya biashara na Allah(s.w) kwa kutarajia pepo hahongeki au hawezi kurubuniwa kwa namna yoyote ile. Wanaohongeka ni wanafiki wanaopenda maisha ya dunia zaidi kuliko ya akhera.(xi) Imekuwa ni tabia ya maadui wa kiislamu, wakiwemo wanafiki,kuwapakazia watu wema makosa mbalimbali na kuwaita majina mabaya ya kuwadhalilisha na kuwafadhehesha ili watu wasiwasikilize na kuwafuata. Hufanya hivyo ili kujenga mazingira ya kuwapoteza watu na Dini ya Allah(s.w)(xii)Uchawi ni njia ya Shetani na ni haramu kwa muislamu kujifunza na kuifanyia kazi elimu ya uchawi.

- Waislamu wanaelekezwa na Mola wao kuwa mara kwa mara wajikinge na shari za wachawi, mahasidi na shari za viumbe wake wengine wanaoonekana na wasio onekana, kwa kusoma kwa mazinagiatio Suratul-Ikhlas na Al- muwadhatain(Al-Falaq na An-Nas).                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 298


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Haki na wajibu kwa masikini, mafukara na wasio jiweza
Soma Zaidi...

Maana ya swala
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno 'Swalaat' lina maana ya 'ombi au 'dua. Soma Zaidi...

HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

mchango
Soma Zaidi...

Taratibu za mahari katika uislamu
Soma Zaidi...

Sababu za mdomo kuwa mchungu
Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu. Soma Zaidi...

Dhana ya mirathi na kurithi katika zama za ujahiliya
Mirathi katika jamii za kijahiliKatika jamii nyingi za kijahili kama vile jamii ya Waarabu kabla ya Mtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara. Soma Zaidi...

Imam Nasai na kitabu cha Sunan
Soma Zaidi...

Nini maana ya asaba katika mirathi ya kiislamu
Soma Zaidi...

msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango
Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzaziKama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi. Soma Zaidi...

Tafsir ya suratul quraysh na mafuzoyake
Soma Zaidi...