Nabii Ayyuub(a.s) Kutekeleza Kiapo Chake


Mkewe Ayyuub(a.s) alikuwa naye ni mama mcha-Mungu mwenye subira. Alimuuguza mumewe kwa kipindi kirefu kiasi hicho katika hali ngumu bila ya kuchoka. Lakini inasemekana siku moja aliteleza na kutamka maneno ambayo yalimchukiza Nabii Ayyuub(a.s) kwa kuwa yalikuwa yanamtoa katika imani ya Allah(s.w). Inasemekana mkewe aliteleza na kusema, “Hivi huu ugonjwa utaendelea mpaka lini?” Nabii Ayyuub(a.s) alimkemea mkewe juu ya kauli yake hiyo na kumuahidi kuwa akipona atamuadhibu kwa kumcharaza bakora mia.Baada ya Nabii Ayyuub(a.s) kupona, Allah(s.w) alimuelekeza namna yakutekeleza kiapo cha kumuadhibu mkewe aliyemfanyia ihsani na kuvumilia shida kiasi kile, kwa maelekezo ya Allah(s.w) hakupaswa kumcharaza bakora mia, bali aliagizwa achukue vijiti mia avifunge pamoja kisha ampige navyo mara moja kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
“Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, (si fimbo); kisha mpige kwacho (mkeo kwa kiapo ulichoapa kuwa utampiga kwa mabaya aliyoyafanya), wala usivunje kiapo.” Bila shaka tulimkuta ni mwenye subira, mja mwema; kwa hakika alikuwa mnyenyekevu sana. (38:44)