Dua ya Ayyuub(a.s)


Nabii Ayyuub(a.s) aliendelea na maradhi yale mazito kwa kipindi kirefu (ina semekana miaka saba). Mwishowe akaona amuelekee Mola wake na kumuomba amuondolee maradhi yale kama tunavyojifunza katika ya zifuatazo:
Na (Mtaje) Ayyubu, alipomwita Mola wake (akasema) “Mimi imenipata dhara, nawe ndiwe Unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.” (21:83)

Dua ya Ayyuub(a.s) ilikuwa makubuli kwa Mola wake kumuelekeza dawa ya matibabu yale:(Mwenyezi Mungu akamwambia):- “Uharikishe mguu wako (patachimbuka chemchem chini yake, maji yake yatakuwa dawa yako). Basi haya maji baridi ya kuogea (koga), na (haya maji baridi) ya kunywa, (yanywe).” (38:42)Baada ya kutumia dawa hii Nabii Ayyuub(a.s) alikuwa mzima wa afya kama alivyokuwa hapo awali kabla ya ugonjwa. Furaha zaidi kwake, pamoja kurudishiwa afya yake, pia alirudishiwa mali na watu wake kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:Basi tukamkubalia (wito wake) na tukamuondolea dhara aliyokuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao. Ni rehema inayotoka kwetu, na ukumbusho (mzuri kwa wafanyao Ibada. (21:84)Na tukampa watu wake na wengine kama wao pamoja nao, kwa rehema itokayo kwetu, na (ipate kuwa) mauidha kwa watu wenye akili. (38:43)