Mafunzo yatokanayo na maandalizi ya mtume ki-wahay


image


Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)


Mafunzo yatokanayo na Maandalizi ya Mtume (s.a.w) Kimafunzo 

        (Ki-wahay).

  1. Elimu katika fani zote (isipokuwa uchawi) ndio nyenzo kuu katika maandalizi kuusimasha Uislamu katika jamii.

 

  1. Kisimamo cha usiku kufanya ibada, ni katika nyenzo kuu ya pili katika maandalizi ya kusimamisha Uislamu katika jamii.

 

  1. Kusoma Qur’an kwa mazingatio kwa lengo la kuifanya muongozo pekee wa maisha pia ni maandalizi ya kuutawalisha Uislamu katika jamii.

 

  1. Kumtaja na kumtukuza Allah (s.w) vilivyo, pia ni katika nyenzo na maandalizi katika kuusimamisha Uislamu ndani ya jamii.

 

  1. Kujitupa kwa Allah (s.w) kwa kweli – ni kumcha Allah (s.w) peke yake ukweli wa kumcha, nayo ni katika maandalizi ya kusimamisha Uislamu.

Rejea Qur’an (3:102).

 

  1. Kumfanya Allah (s.w) ndiye mlinzi pekee na kumtegemea, ni jambo la muhimu katika kusimamisha Uislamu katika jamii.

 

  1. Kusimama na kuonya (kulingania Uislamu), ni jambo muhimu sana linalowezesha Uislamu kufahamika kwa watu.

 

  1. Kutakasa (kutwaharisha) nguo ni amri ya Allah (s.w) inayomtaka kila mlinganiaji wa Uislamu kuwa safi wa kuigwa kimwili na kiroho pia.

Rejea Qur’an (41:33).

 

  1. Kupuuza na kujitenga na mabaya na wabaya ni jambo la muhimu ili kukataza kwake maovu kuwe na athari.

 

  1. Kufanya ihsani (wema) kwa ajili tu kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w) ndio uhai wa ibada ya muislamu.

 

  1. Kufanya subira kwa ajili ya Allah (s.w) ni katika nyenzo kuu katika kupelekea kuusimamisha Uislamu katika jamii.

 

  1. Utekelezaji wa ujumbe wa Qur’an ni kazi nzito na yenye kila aina ya misukosuko, hivyo kuwa na subira ndio nyenzo pekee.


 

  1. Mtume (s.a.w) Kuulingania Uislamu Makkah kwa siri.

-    Mtume (s.a.w) alianza kulingania familia yake, kisha rafiki zake na jamaa zake wa karibu walio rafiki.

 

-    Mtume (s.a.w) alianza kulingania Uislamu kwa siri kwa muda wa miaka mitatu kwa kukutana na waislamu waliosilimu mwanzo kabisa katika nyumba ya bwana Arqam bin Arqam – maarufu kama Darul-Arqam.

 

 

  • Mtume (s.a.w) kuutangaza Uislamu Makkah kwa jamii nzima.

-    Baada ya miaka mitatu ya kuulingania Uislamu kwa siri, aliamrishwa kuutangaza sasa hadharani kwa jamii yote inayomzunguka. 

 

-    Mara tu baada ya Mtume (s.a.w) kuutangaza ujumbe wa Uislamu hadharani, alikumbana na Upinzani dhidi ya ujumbe wake huo kutoka kwa Makafiri wa Kiqureish wa Makkah.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    3 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Namna lengo la zakat linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Umuhimu wa funga ya ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Maswali juu ya Sunnah na hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Matendo ya hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mafunzo kutokana na vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kuamini siku ya mwisho
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

image Mafunzo ya sura zilizochaguliwa
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Sababu za kutokubalika kwa vitabu vilivyotumwa kuwa muongozo sahihi wa maisha ya mwanadamu zama hizi
Soma Zaidi...