image

Vipengele vya Mikataba ya ‘Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina

Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A.

Vipengele vya Mikataba ya ‘Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina

Vipengele vya Mikataba ya ‘Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina


Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A.D, walikuja kama wageni wa Mtume(s.a.w) Waislamu 12 kutoka Yathrib, 10 kutoka katika kabila la Khazraj na 2 kutoka katika kabila la Aus.Katika hawa 12, Waislamu 5 walikuwa katika wale waliosilimu mwaka uliopita na 7 walikuwa wapya. Walimuomba Mtume(s.a.w) awapelekee mtu wa kuwafundisha Uislamu na kuutangaza Uislamu kwa watu wa Yathrib. Mtume(s.a.w) alikubali ombi lao na akampeleka huko Mus’ab bin ‘Umair. Baada ya Hija Mtume(s.a.w) aliagana na wale wageni na akawataka watoe ahadi mbele yake kuwa:


(i) Hawataabudu chochote kingine ila Allah pekee.

(ii) Hawataiba wala hawatapokonya misafara njiani.

(iii)Hawatazini.

(iv)Hawatawaua watoto wao tena.

(v) Hawatasema uwongo wala hawatawasingizia watu wengine uovu.

(vi)Hawatamuasi Mtume kwa kila atakalowaamrisha na watakuwa waaminifu kwake kwa hali yoyote iwayo.Huu unajulikana kama mkataba wa kwanza wa ‘Aqabah uliokuwa kati ya Mtume(s.a.w) na wale wageni 12 wa Yathrib. Waliporejea Yathrib walitekeleza ahadi ile na muda si mrefu watu wengi wa kabila la Aus na Khazraj walisilimu.Labda ni vyema tujiulize ni kwanini waarabu wa Yathrib waliitkia wito wa Mtume(s.a.w) kwa wepesi kiasi hicho ambapo waarabu wengine wote walikuwa wagumu sana. Bila shaka ni kutokana na historia ya Yathrib yenyewe. Tumeona kuwa Yathrib ilikaliwa na mchanganyiko wa Mayahudi na waarabu.Waarabu wa Yathrib hawakuwa wamezama sana katika kuyaabudu masanamu kutokana na athari ya mafundisho ya Dini ya kiyahudi na baadhi ya waarabu waliacha Dini za wazee wao na kufuata Dini ya kiyahudi. Pia waarabu wa Yathrib walizoea kusikiakutoka kwa Mayahudi juu ya Utabiri wa kuja kwa Mtume na dalili zake. Hivyo walipokutana na Mtume(s.a.w) na kumuuliza maswali mbali mbali yaliyowapelekea kuhakikisha zile alama za Utume wake na Mtume(s.a.w) akawajibu maswali yao vilivyo, walidhihirikiwa kuwa bila shaka yeye ndiye yule Mtume aliyetabiriwa katika vitabu vya Mayahudi. Ajabu ni kwamba Mayahudi wenyewe hawakumkubali Mtume(s.a.w) na waliungana na washirikina kumpiga vita .Hija iliyofuatia, mnamo Machi 622 A.D, walimjia Mtume(s.a.w) Waislamu 75 kutoka Yathrib, wawili wakiwa wanawake, wakiongozana na mwalimu wao, Mus’ab bin ‘Umair. Baada ya Hija Mtume(s.a.w) alikutana na kikundi hiki cha Waislamu usiku wa manane katika sehemu ya siri nyuma ya mlima. Kutoka Makka Mtume aliongozana na Abubakar, Aly na ami yake Abbas (ambaye alikuwa bado hajasilimu). Mtume(s.a.w) alitoa khutuba ndefu, akiwasomea aya za Qur-an na kuwatofautishia Uislamu na Ukafiri. Kisha akawataka wamuahidi kuwa akienda kwao watamuhifadhi yeye na wafuasi wake kama wanavyowahifadhi watoto wao na wake zao wakati wa vita. Aliposikia ombi hili, Barq bin Marur, aliyekuwa mkubwa wao, alisimama na kumhakikishia Mtume(s.a.w) kwa niaba ya watu wake kuwa wako tayari kumlinda Mtume na watu wake. Kabla ya kufunga mkataba wa ahadi ya kumlinda Mtume(s.a.w), Abbas, aliwaomba watafakari na kuelewa vizuri uzito wa ahadi wanayotaka kuichukua na kuwaambia:“Enyi watu wa Khazraj! Mnaifahamu nafasi aliyoshika Muhammad hapa kwetu. Tumekuwa tukimlinda na shari za watu wetu kwa kadiri tulivyoweza. Ni mtu mwenye kuheshimiwa sana na wafuasi wake na yuko salama kabisa hapa. Sasa mnataka akaishi nanyi huko kwenu. Kama mnafikiri mnaweza kutekeleza kama mnavyoahidi kwamba mtamlinda kwa namna yoyote iwayo, basi mnaweza kumchukua vinginevyo ni vema mumuache hapa”16.Barq bin Marur alisimama tena na kusisitiza kuwa wako tayari kumlinda Mtume na watu wake kwa nafsi zao, mali zao, wake zao, watoto wao na kwa nyumba zao. Baada ya kutoa ahadi hii kila mmoja katika wale wanaume 73 alimpa Mtume mkono wa ahadi(Bai’ayah),Barq akiwa ndiye wa kwanza kumpa Mtume(s.a.w) mkono.Huu ni mmkataba wa pili wa ‘Aqabah. Kisha Mtume(s.a.w) aliwachagua viongozi 12, 9 kutoka katika kabila la Khazraj na 3 kutoka katika kabila la Aus. Kila kiongozi alimpa ukoo utakaokuwa chini ya uongozi wake. Jukumu kubwa la viongozi hawa lilikuwa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuishi Kiislamu. Baada ya hapo walimuaga Mtume na kumsisitizia kuwa wanamngojea yeye pamoja na Waislamu kwa hamu kubwa.Mafunzo Yatokanayo na Mikataba ya ‘Aqabah
Tunajifunza yafuatayo kutokana na mikataba ya ‘Aqabah:
Kwanza, Waislamu wanapoazimia kufanya jambo au kuchukua njia fulani itakayowapelekea kusimamisha Uislamu hawanabudi kujifunga katika utekelezaji wa azimio hilo kwa kupeana kiapo cha ahadi. Kiapo cha ahadi kitawalazimisha kutekeleza azimio lile wakikumbuka kuwa:


Kwa hakika ahadi itaulizwa (Siku ya Kiyama) (17:34)
Bila shaka wale wanaofungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Basi avunjaye ahadi (hizi) anavunja kwa kudhuru nafasi yake; na atekelezaye aliyomuahidi Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu) atamlipa ujira mkubwa.(48:10)Hivyo, kwa kujua uzito wa ahadi, hapana budi kwa kila mwenye kuchukua ahadi ya utekelezaji wa azimio fulani, kuvifahamu vyema vipengele vya azimio hilo, ugumu wa utekelezaji wake na athari yake baada ya utekelezaji kabla hajachukua ahadi ya kulitekeleza. Muislamu asije kujichukulia tu ahadi ya kutekeleza jambo bila ya kujua vyema dhima anayoichukua.Pili, tunajifunza pia kuwa Waislamu wanapopanga mambo yao hawanabudi kuhakikisha kuwa wanayapanga kwa siri ili wasijejulikana kwa maadui zao hata kabla ya kuanza kuyatekeleza. Mtume(s.a.w) alikutana na wale Waislamu 75 kutoka Yathrib katika sehemu ya siri usiku wa manane, si Waislamu wote wa Makkah waliohusika. Makka iliwakilishwa na watu wanne tu, Mtume mwenyewe, Abubakar, Aly na Abbas, wote hawa watatu wakiwa ni wandani wa Mtume(s.a.w)Usiri huu ulisaidia sana wakati wa kuhamia Madinah. Maquraish walistukia kuhama kwa waislamu baadaye kabisa, baada ya watu wengi kuhama. Kuhama kwenyewe kulifanyika kwa siri sana.Tatu, tunajifunza kuwa katika kusimamisha Uislamu uongozi bora ni kitu cha msingi na cha awali. Tumeona kuwa hata kabla hajahamia Madinah, Mtume(s.a.w) aliteua viongozi wa kumsaidia kuwaweka sawa watu wa Madinah kwa kuwaelimisha juu ya Uislamu na juu ya majukumu yao kama Waislam. Uongozi bora wa Kiislamu ulijenga umoja miongoni mwa watu wa Madinah na hii ilisaidia sana katika kuanzisha Dola ya Kiislam Madinah.

                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 274


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Katika Mji wa Taif
Baada tu ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Maandalizi ya hijrah ya mtume na waislamu kuhamia madinah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

HISTORIA YA WATU WAOVU WAKIOTAJWA KWENYE QURAN
Soma Zaidi...

Uchaguzi wa Ali bin Abu Twalib kuwa Khalifa wa nne na chanzo cha Makundi katika Uislamu
Soma Zaidi...

Maswali kuhusu Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD
Baada ya Nuhu(a. Soma Zaidi...

Maryam Apewa Habari ya Kumzaa Isa(a.s)
Baada ya maandalizi hayo ya kimalezi pamoja na hifadhi ya Allah(s. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Bani Israil
Soma Zaidi...

Upinzani Dhidi ya Dola ya Kiislamu Wakati wa Makhalifa
Soma Zaidi...

Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa Polisi na magereza kati uislamu wakati wa Makhalifa
Kuanzishwa kwa Polisi. Soma Zaidi...