image

Historia ya maimam Wanne wa fiqh

Historia ya maimam Wanne wa fiqh

Maimamu Wanne wa Fiq-hiPamoja na kutokea mara kwa mara viongozi wema waliojitahidi kuirejesha jamii ya Kiislamu katika sura yake asilia, kama alivyojitahidi ‘Umar bin Abdul Aziz, viongozi wengi waliendelea kuutawala ulimwengu wa Waislamu kwa kuimarisha Ufalme na Udikteta zaidi kuliko Uislamu. Lakini, pamoja na kuwepo hawa watawala waovu, bado palikuwepo watu wema katika miji mbali mbali ya Dola hizo za Kifalme. Kwamfano, mji wa Baghdad ulijaa watu ambao walikamatana na Uislamu. Aidha walikuwepo viongozi wa dini ambao, pamoja na kutotambuliwa na watawala, walisimama imara kuwaongoza Waislamu. Pamoja na maguvu na vyombo vya Dola vya kutisha walivyokuwanavyo watawala bado, raia waliwaheshimu na kuwatii zaidi viongozi wao wa kiislamu.


Katika kupanuka dola ya Kiislamu, tangu wakati wa Makhalifa wanne wa Mtume(s.a.w), matatizo kadhaa yaliibuka ambayo yalihitaji ufumbuzi. Dola ilipanuka toka mashariki ya kati hadi Asia yote, sehemu za Afrika ya kaskazini na Hispania (Spain) huko Ulaya. Yaliibuka matatizo ya kisheria, taratibu za kibiashara na uchumi kwa ujumla na mila na desturi za watu mbalimbali . Uislamu ulitakiwa utoe fa-twa. Vinginevyo zingeibuka sheria na kanuni tofauti na Uislamu. Juhudi za mwanzo zilizofanywa ilikuwa ni utungaji na utoaji wa Fat’wa juu ya masuala mbalimbali kulingana na Qur’an na Sunnah. Hiki ndicho kipindi cha “Tabiina” ambacho waliibuka Maimamu wanne waliotumia uhai wao wote katika kutoa ufafanuzi, rai na Fat’wa juu ya sheria za Kiislamu katika mas’ala mbalimbali ya maisha. Hawa ni mabwana: Nu’man Ibn Thabit Abu Hanifa, Malik Ibn Anas, Muhammad Ibn Idris al- Shafii na Abu Abdallah bin Muhammad Ahmad Ibn Hambal. Wote hawa walitoa mchango mkubwa sana katika sheria ya Kiislamu na walikubaliana katika mambo yote ya msingi (Usul). Hawakufarakana kwa tofauti za maoni zilizojitokeza katika mambo madogo madogo.


Imam Abu Hanifa (80-150 A.H) na Imam Malik Ibn Anas (93-179 A.H) walirithi elimu ya moja kwa moja toka kwa masahaba iliyoegemea Qur’an na Sunnah. Aidha wao wenyewe walifanya juhudi kuongeza ujuzi wao kulingana na mazingira mapya yaliyokuwa yakijitokeza.


Imam Shafii (150 - 204 A. H) aliendeleza juhudi za Abu Hanifah na Malik kwa kufanya utafiti zaidi wa ukusanyaji na uchujaji wa Hadith, na maoni ya wataalamu mbalimbali wa sheria.


Imam Ahmad bin Hambal (164-204 A.H) aliandika Musnad ambacho ndicho kitabu mashuhuri kabisa cha Sunnah.Maimamu wote hawa ama wamesoma na kufundishana au kusoma kwa Waalimu sawa. Imam Malik na Abu Hanifa wote walisoma Hadith kutoka kwa Imam Muhammad Ibn Shihab al-Zuhr.


Imam J’afar al-Sadiq aliwahi kuwa mwalimu wa wote Imam Abu Hanifa na Imam Malik. Aidha, wote hawa walisomeshwa pia na “Tabii” mashuhuri Muhammad bin al-Mukadir al-Madani.


Imam Abu Hanifah pamoja na utu uzima wake, alikuwa akihudhuria darasa hasa la Hadith la Imam Malik. Imam Shafii pia alisoma kwa Imam Malik. Kwa ujumla Maimamu wote wanne walihusiana sana katika kusoma kwao na japo walitofautiana katika maoni juu ya mambo kadhaa, walikuwa wamoja katika Uislamu na wakiheshimiana.


Hivi leo wapo watu wanaojinasibisha na madhehebu ambao hudai yapo madhehebu manne ndani ya Sunni wal-Jamaa, kila madhehebu ikinasibishwa na mmoja wa Maimamu hao wanne. Na japo haisemwi wazi wazi, lakini zipo hisia kwa mfano wanaojiita Shafii kuwaona wale wa Hambal, Hanafi na Malik kuwa hawapo sawa. Pengine na kinyume chake. Lakini hakika ya mambo na ushahidi wa vitabu vya historia haioneshi popote mabwana hawa kuhusika na fikra hizi za kuwa na madhehebu yasiyochanganyika. Kazi yao kubwa waliyofanya ni kutoa ufafanuzi wa kifiqh juu ya mas’ala mbalimbali na sio kuwagawa Waislamu kwenye madhehebu. Katika Uislamu suala la madhehebu ni uzushi. Labda ni vyema tuangalie kwa ufupi maisha na mchango wa kila Imam katika kuhuisha Uislamu.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 931


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII SULEIMAN
Soma Zaidi...

NINI MAANA YA SWALA (SALA AU KUSWALI), KILUGHA NA KISHERIA KATIKA UISLAMU
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua. Soma Zaidi...

TAREKH, HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
1. Soma Zaidi...

NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA) BINTI KHUWALD
MTUME Muhammad (s. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SALIH(A.S
Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Juhudi za Waislamu Katika Kuhuisha Harakati za Kiislamu Zama za Nyerere hadi leo
i. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUT(A.S) NA WATU WA SODOMA NA GOMORA
Mtume Lut(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME DAUD(A.S).
Nabii Daudi(a. Soma Zaidi...

Uasi katika dola ya kiislamu na matokeo yake
Uasi katika dola ya kiislamu na matokeo yake. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ayyuub(a.s)
Kutokana na kisha hiki cha Nabii Ayyuub(a. Soma Zaidi...

Kusingiziwa Nabii Sulaiman Uchawi
Pamoja na Ucha-Mungu aliokuwa nao Nabii Sulaiman watu hawakuacha kumsingizia mambo machafu. Soma Zaidi...

Kifo cha Khalia Uthman kilivyotokea
Soma Zaidi...