Ukombozi wa mji wa Makka (Fat-h Makka) mwaka 8 A.
Ukombozi wa mji wa Makka (Fat-h Makka) mwaka 8 A.H. uliwezesha Uislamu kuenea kwa kasi kubwa Uarabuni kote. Nchi jirani za wakristo, hasa katika Himaya ya Warumi, zilishikwa na wivu mkubwa kutokana na kuimarika kwa Uislamu hasa kwa kasi kubwa kiasi kile. Pia waliona hatari iliyopo mbele yao kutokana na kuibuka nguvu kubwa ya Uislamu. Waliona hapana budi kuandaa mashambulizi ya nguvu ili kupunguza kasi ya nguvu ya Uislamu.
Hivyo, Warumi chini ya uongozi wa Heracleus, waliandaa jeshi kubwa sana dhidi ya Dola ya Kiislamu, wakishirikiana na nchi nyinginezo za wakristo.
Kama kawaida yake, Mtume(s.a.w) alipohakikisha juu ya maandalizi ya Warumi na nchi za Kikristo dhidi yake, hakusubiri mpaka wamvamie, bali aliandaa jeshi kubwa la Waislamu na kuelekea Syria kupambana na jeshi la Warumi.
Baada ya wiki mbili (siku 14) jeshi la Waislamu lilipiga kambi. Tabuk, mji ulioko kati ya Madinah (mji mkuu wa Dola ya Kiislamu) na Damascus (mji mkuu na mkongwe wa Syria), likingojea lisikie zaidi juu ya miondoko ya jeshi la maadui. Warumi walipopata habari juu ya maandalizi ya kivita ya Mtume(s.a.w), wakikumbuka matokeo ya vita vya Muttah, waliogopa na kurudi ndani ya mipaka yao.
Kwa kuwa lengo la jeshi la Mtume(s.a.w) lilikuwa kuihami Dola ya Kiislamu na wala sio kuvamia Syria, alibakia pale Tabuk, kilometa 700 kutoka Madinah, na kuendelea na kazi ya Daโawah. Makabila mengi ya Wakristo yalijisalimisha kwa dola ya Kiislamu na kuwa tayari kulipa Jizya. Huo ukawa ndio mwisho wa โU-super powerโ wa dola ya Kirumi na Uislamu ukachukua nafasi yake na kutimia neno la Allah(s.w):
Yeye ndiye aliyemtuma, (aliyemleta) Mtume wake kwa uwongofu na dini iliyo ya haki, ili ishinde juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi. (48:28)
MafunzoYatokanayo na Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu.
Kwanza, kila Uislamu unavyopiga hatua ya maendeleo ndivyo maadui wake wanavyozidi kuwa wengi na kujiimarisha. Katika kipindi cha Makkah, ambapo Waislamu walikuwa katika hali ya udhaifu, adui alikuwa mmoja tu, Makafiri wa Kiquraish. Katika kipindi cha Madinah ambapo Dola ya Kiislamu ilianzishwa na kuendelea kila uchao, maadui nao waliongezeka mpaka ikabidi Waislamu waingie vitani kupambana na kuwashinda maadui watano walioainishwa.
Pili, Waislamu watakapojitahidi kupigania Uislamu kwa kadiri ya uwezo wao kwa kutoa mali zao na nafsi zao, Allah atawawezesha kupata ushindi kwa hali yoyote iwayo.
Tatu, Siri ya mafanikio ya Waislamu ya kusimamisha na kuendeleza Dola ya Kiislamu ni kule kumtii kwao Allah(s.w) na Mtume wake katika kila waliloamrishwa na kila walilokatazwa kwa shauku kubwa ya kupata radhi za Allah(s.w) na kuepukana na ghadhabu zake.