Mapambano ya Dola ya kiislamu dhidi ya maadui wa kikristo (warumi) wakati wa Mtume

Mapambano ya Dola ya kiislamu dhidi ya maadui wa kikristo (warumi) wakati wa Mtume

Mapambano ya Dola ya kiislamu dhidi ya maadui wa kikristo (warumi) wakati wa Mtume

Warumi (Wakatoliki)


Warumi mpaka kufikia 7 A.H. sawa na 629 A.D. walikuwa ni Taifa kubwa (super Power) lililokuwa likitamba kwa nguvu za kishindo katika ulimwengu wa wakati huo. Baada ya mkataba wa Hudaybiyah Mtume(s.a.w) alituma wajumbe katika nchi mbali mbali za ndani na nje ya Bara Arabu. Miongoni mwa watawala waliopelekewa ujumbe na Mtume(s.a.w) ni mfalme wa Basra aliyepelekewa barua na Haarith bin ‘Umar Azid. Haarith alipofika Muttah aliuliwa na Shurahbil Ghassaany aliyekuwa Gavana wa Dola ya Kirumi chini ya Mfalme Heracleus.



Kumuua mjumbe lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa sheria ya makabila ya Kiarabu wakati ule. Hivyo , Mtume(s.a.w) alipopata habari ya kuuliwa mjumbe wake, aliandaa jeshi la watu 3,000 chini ya Uamiri wa Zaid bin Harith kwenda Muttah kupambana na Gavana wa Warumi, Shurahbil Ghassaany. Wakati Mtume anatuma jeshi hili aliagiza:



“Kama Zaidi atauliwa, Ja’far bin Aby Taalib atakuwa Kamanda wenu, na kama naye atauliwa, ‘Abdullah bin Rawahah atachukua ukamanda. Kama naye atakufa mumchague kamanda kutokana na nyinyi.”



Shurahbil alipopata habari za kuja kwa jeshi la Waislamu aliandaa jeshi la askari laki moja (100,000) Jeshi la waislamu lilipofika njiani lilipata uvumi kuwa Heracleus anakuja na jeshi lingine la askari 100,000. Jeshi la Waislamu lilisita njiani siku mbili ili kuweka mikakati ya namna ya kupambana na jeshi kubwa kiasi hicho. Baada ya kushauriana Waislamu wote 3,000 katika kikosi kile waliamua kupambana na maadui zao na maadui wa Allah(s.w) kwa gharama yoyote ile.



Zaid aliongoza vita na mapambano makali yakaanza. Si muda mrefu kaka wa Shurahbil aliuliwa na yeye mwenye akakimbilia mafichoni kwenye ngome. Shurahbil alituma ujumbe kwa Mfalme Heracleus ambaye mara tu alituma jeshi lenye nguvu la askari 100,000 kujiunga katika mapambano dhidi ya Waislamu
3,000 tu. Waislamu wachache sana (3,000) wakawa wanapigana na jeshi kubwa sana (200,000) lenye nguvu na uzoefu wa vita. Uwiano wa jeshi la Waislamu na jeshi la Warumi ulikuwa 3,000:200,000 = 3:200 ni sawa na1:67


Zaid bin Harith aliuliwa na Ja’afar akachukua nafasi yake. Naye alipiganisha kwa ushujaa mpaka akafa shahidi. Baada ya Ja’afar, ‘Abdullah bin Rawahah alichukua bendera ya vita naye akafa shahidi. Baada yake Waislamu walimchagua Khalid bin Walid kuwa kamanda wao. Waislamu chini ya uongozi wa Khalid waliendelea kupigana kwa ushujaa mkubwa. Katika mchana mmoja wa mapigano Khaild alichakaza panga nane na katika usiku wake, ilibidi Warumi waombe kuakhirisha vita mpaka kesho yake.



Siku iliyofuatia Khalid aliwapanga askari wake katika mstari mrefu kama vile anataka kuwazingira maadui na kuwaweka katikati. Warumi waliogopa kujitokeza kwenye uwanja wa mapambano siku ile. Naye Khalid kama mbinu ya kivita, alilirejesha jeshi lake Madina. Warumi walifurahi sana kuona vita vimekwisha, kwani hawakuwa na nguvu tena ya kupambana na Khalid. Kwa upande mwingine, Waislamu wa Madina hawakufurahishwa na kitendo cha jeshi la Waislamu kuacha mapigano na kurudi Madinah bila ya kupata ushindi. Waliwatupia michanga ya usoni huku wakiwasimanga.

“Enyi mliokimbia vita! Mnakimbia njia ya Allah”!



Mtume(s.a.w) aliwaliwaza na kujibu mashambulizi kwa niaba yao, “Sio wakimbizi, Inshaa Allah watarudi tena”. Ni kweli kuwa hawakuwa na dhamira ya kukimbia vita bali walirejea Madina ili kukusanya nguvu upya. Mtume(s.a.w.) na Waislamu walipata majonzi makubwa kwa kuwapoteza mashujaa wengi na hasa wale makamanda watatu.



Mafunzo Yatokanayo na Vita vya Muttah


Waislamu hawakufurahia kuwaona wenzao wanarudi bila ya ushindi. Kwa Waislamu, walikuwa na mawili tu ya kupata katika vita, ushindi au kufa shahidi katika njia ya Allah. Hawakuzoea kabisa kurudi nyuma, ila iwe kama mbinu ya kivita ili kutafuta nguvu zaidi kama alivyofanya Khalid ambayo inaruhusiwa:
“Enyi mlioamini! Mkutanapo vitani na wale waliokufuru basi msiwageuzie migongo (mkakimbia). (8:15)




Na atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo – isipokuwa amegeuka kwa kushambulia au amegeuka akaungane na sehemu nyingine ya jeshi hili hili la Waislamu (ikiwa si hivyo) – atastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na mahali pake ni Jahanamu. Napo ni mahali pabaya pa kurejea (mtu). (8:16)



Wakristo katoliki (Warumi) hawakujiona kuwa wameshinda wala kushindwa. Hawakushinda kwa sababu wao ndio waliogopa kukabiliana na Waislamu na wakakataa kujitokeza kwenye uwanja wa mapambano. Hawakushindwa kwa sababu Waislamu hawakuendelea kupambana nao mpaka kuwafikisha katika kilele cha kushindwa. Hata hivyo Warumi (Wakristo) walishangazwa sana na ushujaa wa Waislamu. Waliona kuwa ni jambo la hatari kubwa kupigana na Waislamu ambao walishambulia kama simba na kila mmoja alikuwa kama vile ana maisha mengi (uhai mwingi).



Walishuhudia nguvu za Waislamu kwa mifano waliyoipata kwa watu kama Ja’far ambaye aliendelea kupigana baada ya mikono yake yote miwili kukatwa; na Khalid ambaye alichakaza panga nane katika kipindi kifupi cha mchana mmoja wa mapambano. Hivyo, walishafikia hatua ya kukata tamaa na walipendelea kuomba suluhu lakini kutokana na kibri chao waliona haya kufanya hivyo. Kwa hiyo walifurahi sana walipoona Waislamu wenyewe wameamua kuondoka na hawakuamini macho yao.



Kwa upande mwingine, Mayahudi na washirikina walifurahi sana kwa msiba uliowapata Waislamu. Walifikia hatua ya kujiwa na mawazo kuwa nuru ya Uislamu itazimwa na Wakristo (Warumi). Wakati vita baina ya Waislamu na Warumi vinaendelea, Mayahudi na washirikina walikuwa wakifanya njama za kuwahujumu Waislamu.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Download App yetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 786

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Vita vya Al Fijar na sababu zake

Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar.

Soma Zaidi...
tarekh 06

MAISHA YA UTOTONI YA MTUME S.

Soma Zaidi...
tarekh 02

FAMILIA YA MTUME (S.

Soma Zaidi...
Si Yesu Aliyesulubiwa (yesu hakufa msalabani wala hakusulubiwa

Katika Qur,an tukufu, Mwenyezi Mungu aliye muweza na mjuzi wa mambo anathibitisha kuwa aliyesulubiwa si Nabii Isa(a.

Soma Zaidi...
Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume

Uchaguzi wa ‘Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.

Soma Zaidi...