Menu



tarekh 10

KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.

KULELEWA NA BABA YAKE MDOGO
Baada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Kiongozi ambaye alikabidhiwa mamlaka ya kukichimba upya kisima cha zamzam baada ya kufukiwa na watu kutoka kabila la Jurhum pindi walipoondoka Makkah. Alisimama Abu Talib kumlea mtoto wa ndugu yake. Kwani huyu ndiye aliyekuwa mtoto mkybwa wa Abdul al-Muttalib.

Abu Talib alimpenda sana kijana wake zaidi ya anavyowapenda watoto wake. Mtume (s.a.w) alikuwa ni mwenyekuridhika kwa kile ambacho alikuwa akikipata. Allah alimuongezea rizk mzee Abu Talib. Mzee huyu alimlea kijana wake Mpaka alipofika umri wa miaka arobaini. Watu walimpenda kijana Muhammad jinsi alivyokuwa na tabia njema na uaminifu.

Watu wa Makkah walikuwa wakiomba mvua kupitia utukufu wake. Imesimuliwa kutoka kwa Ibn ‘Asakir kuwa Jalhamah bin Arfuta kuwa amesema nilifika Makkah wakati ambao kulikuwa hakuna mvua, Maquraish wakatoka kumueleza mzee Abu Talib kuwa awaombee mvua. Basi akatoka akiwa na kijana chake na akamsimamisha pembeni ya ukuta wa al-kabah kisha akaomba dua. Kwa hakika kulikuwa hakuna mawingu lakini ghafla mawingu yakajikusanya kutoka huku na kule na hatimaye mvua ikanyesha


                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views 300

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Mtume Muhammad s.a.w analelewa na Babu yako ikiwa na umri wa miaka 6

Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 9.

Soma Zaidi...