Mtume Isa(a.
Mtume Isa(a.s.)alipewa Utume na kuamrishwa kufikisha ujumbe wa Allah(s.w) kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israil. Akibainisha juu ya jambo hili, Nabii Isa(a.s) alisema: β............Enyi wana wa Israili; Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nisadikishaye yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati na kutoa habari njema ya Mtume atakayekuja nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad. (61:6).
Na katika Biblia tunafahamishwa kuwa Nabii Isa(a.s)alisema kauli hiyo kwamba yeye ni Mtume kwa wana wa Israili tu. Ukweli huu unajitokeza pale Yesu alipojibu, akisema: Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israili(Mathayo 15:21-24)
(i) Mungu ni mmoja,wapekee,si watatu,na yeye si Mungu
Kwanza kabisa, Nabii Isa(a.s) aliwataka watu wamjue na kumuamini Mwenyezi Mungu mmoja aliye wa pekee, na kuwataka wakubali kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akawaambia:
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na ni Mola wenu. Basi mwabuduni. Hii ndiyo njia iliyonyooka (3:51)
Ujumbe huu wa Nabii Isa, unapatikana pia katika Biblia. Nabii Isa amenukuliwa katika Bibilia akifundisha Wana wa Israili kuwa yeye si Mungu, ila ni Mtume, na kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja, wapekee na ndiye Mungu wa kweli.
Na uzima wa milele ndiyo huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. (Yohana 17:3)
Maneno haya ya Nabii Isa(a.s) yanatuonesha ukweli kuwa yeye si mungu, na wale wanaongβangβania kumwita, Yesu ni mungu, hawayafuati mafundisho yake, bali wanafuata uzushi wa mafundisho na maagizo ya wanadamu. Hili analithibitisha Yesu katika Biblia:
Enyi wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,Watu hawa wananiheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao wananiabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.(Mathayo 15:7-9)
(ii) Hakuna dhambi ya asili
Yesu amefundisha kuwa kila mwanadamu huzaliwa akiwa huru pasina tone lolote la dhambi, na kwamba watoto ndio wakuu katika Ufalme wa mbinguni na Ufalme wa mbinguni ni wao.Na hakuna yeyote atakayeingia katika Ufalme wa mbinguni(peponi) ila atakayejitahidi kutotenda maovu, na kujitahidi kufanya mema akawa safi kama mtoto.
Saa ile wanafunzi wake wakamwendea Yesu wakisema, Ni nani basi aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amini, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni. Basi yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni(Mathayo 18:1-4)
Na katika maandiko mengine ya Biblia, tunasoma: Yesu akasema: Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, Ufalme wa mbinguni ni wao(Mathayo19:14)
Kutokana na mafundisho haya ya Yesu, hakuna mtu yeyote muovu atakayeingia katika Ufalme wa mbinguni (Peponi), kwa kuamini kwamba Yesu kafa msalabani kwa ajili ya dhambi zake.
(iii)Waumini wanatakiwa kufuata sheria za Mwenyezi Mungu kwa kuweka Ufalme wake hapa duniani
Nabii Isa(a.s) aliwafundisha watu wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake katika kila kipengele cha maisha yao. Na kwamba njia ya maisha yenye kuleta amani ya kweli na maisha ya furaha ni kufuata sheria za Mwenyezi Mungu na kuacha mafundisho ambayo ni maagizo ya wanadamu. Katika Qur,an tunafahamishwa kuwa aliwaambia Waisraili. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na ni Mola wenu. Basi mwabuduni. Hii ndiyo njia iliyonyooka. (3:51)
Na katika Biblia, amenukuliwa akiwataka watu wamuombe Mwenyezi Mungu awezeshe Ufalme wake ustawi duniani kama ulivyo stawi mbinguni ili dunia isitawaliwe na kuongozwa kwa sheria zistawishazo ufuska na ufisadi katika jamii. Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni; Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, hapa duniani kama mbinguni (Mathayo 6:9-10)
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 760
Sponsored links
π1 Simulizi za Hadithi Audio
π2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
π3 Kitabu cha Afya
π4 Madrasa kiganjani
π5 Kitau cha Fiqh
π6 kitabu cha Simulizi
Maandalizi ya Hijra ya Mtume na Mafunzo tunayoyapata kutoka katika hijra hii
Maandalizi ya Hijra ya Mtume (s. Soma Zaidi...
HISTORIA YA FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 02. Soma Zaidi...
Maandalizi ya hijrah ya mtume na waislamu kuhamia madinah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kuchimbwa upya kwa kisima cha Zamzam
Sura na historia ya mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 3.Hapa utajifunza kuhusu kufukuliwa kwa kisima cha Zamzam baada ya kufukiwa muda mrefu. Soma Zaidi...
fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...
CHANZO CHA VITA VYA VITA VYA AL-FIJAR NA ATHARI ZAKE
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU). Soma Zaidi...
Kuanzishwa kwa Tawala za kifalme baada ya uongozi wa Makhalifa.
Kuanzishwa Ufalme. Soma Zaidi...
Imam Ibn Majah na Sunan Ibn Majah
Soma Zaidi...
Nabii Ibrahiim(a.s) Kumlingania Uislamu Baba Yake
Baada ya NabiiIbrahiim(a. Soma Zaidi...
Kuanzishwa kwa Polisi na magereza kati uislamu wakati wa Makhalifa
Kuanzishwa kwa Polisi. Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Isa(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Isa(a. Soma Zaidi...
Kuandaliwa Mtume(s.a.w) maandalizi ya kimafunzo na maandalizi ya ki ilham
Mitume huzaliwa Mitume. Soma Zaidi...