Nabii Isa(a.s) Azungumza Akiwa Mtoto Mchanga


Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba. Watu wakastaajabu na kuwaza, imewezekanaje Maryam asiye mzinzi kumpata mtoto bila kuolewa. Na wengine wakauliza:...............“Ewe Maryam! Hakika umeleta jambo la ajabu: Ewe dada yake Haruni! Baba yako hakuwa mtu mbaya wala mama yako hakuwa hasharati (19:27-28)

Kwa maswali hayo, ikawepo haja ya kumtakasa Maryam kuwa japo hakuolewa, hakumpata mtoto huyo kwa zinaa. Ndipo ikatimia kauli ya Allah(s.w) kuwa Nabii Isa(a.s) atazungumza akiwa kichanga.Maryam akaashiria kwake (yule mtoto wamuulize yeye). Wakasema:“Tutazungumzaje na aliye bado mtoto kitandani? (19:29)(Yule mtoto) akasema: “Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu, Amenipa kitabu na Amenifanya Nabii. Amenifanya mbarikiwa popote nilipo. Na ameniusia swala na zaka maadamu ni hai. (19:30-31)Na ameniusia kumfanyia wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, muovu. Na amani iko juu yangu siku niloyozaliwa, siku nitakayokufa na siku nitakapofufuliwa kuwa hai(19:32-33)