Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Mafunzo yatokanayo na Upinzani wa Maquraish dhidi ya Uislamu (Qur’an).
- Upinzani wa Makafiri dhidi ya ujumbe wa Uislamu upo nyakati na muda wote na hautaisha.
- Hatuna budi kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa kuanzia familia, ndugu na jamaa zetu wa karibu kabla ya wengine ili kupata wasaidizi wa karibu.
- Waislamu hawana budi kuwa tayari na kutokata tamaa katika kuusimamisha Uislamu bila ya kumchelea yeyote yule.
- Makafiri siku zote wako tayari kutumia kila mbinu na njia kuhakikisha kuwa wanabaki katika utawala na itikadi za ibada zao ili kuendeleza na kuimarisha maslahi yao kupitia unyonyaji na ukandamizaji.
- Mbinu za Makafiri za kutaka kuuhilikisha Uislamu na waislamu zinafanana katika zama zote za historia ya maisha ya mwanaadamu.
- Mtume (s.a.w) na maswahaba wake waliweza kuhimili vitimbi vya makafiri na hatimaye kuweza kuusimamisha Uislamu katika jamii ni baada ya wao kufuata na kutekeleza kikamilifu mafunzo ya Qur’an (96:1-5), (73:1-10) na (74:1-7).
- Suala la kuulingania na kuutangaza ujumbe wa Uislamu ni zito, lenye misukosuko na gharama kubwa ya kutoa mali na nafsi (uhai).
- Siku zote makafiri na maadui wengine wa Uislamu hawakotayari kuona Uislamu unasimama katika jamii na waislamu wanautekeleza vilivyo.
- Tusitarajie matunda ya kusimama Uislamu kupatikana kwa muda mfupi na kwa urahisi, kwani linahitaji mipango ya muda mrefu na kujitoa muhanga.
- Wakati wowote Waislamu watakapojizatiti katika kuulingania na kuupigania Uislamu kwa mali na nafsi zao, Allah (s.w) atawapa nusura dhidi ya maadui wao.
Rejea Qur’an (61:8, 10-13).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Share follows: 0 |
Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 web hosting 👉6 Madrasa kiganjani
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 web hosting 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Tukio la kupasuliwa kifua Mtume Muhammad S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 7
Soma Zaidi...Kuanzishwa kwa Polisi na magereza kati uislamu wakati wa Makhalifa
Kuanzishwa kwa Polisi.
Soma Zaidi...HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...KUCHIMBWA UPYA KWA KISIMA CHA ZAMZAMA NA KUNYWA MAJI YA ZAMZAMA KISIMA KILICHO BARIKIWA
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba.
Soma Zaidi...