Kulingania watu wake na Miujiza Aliyoonyesha Nabii Isa(a.s)
Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyewawezesha Mitume na Manabii kufanya miujiza.
Kulingania watu wake na Miujiza Aliyoonyesha Nabii Isa(a.s)
Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyewawezesha Mitume na Manabii kufanya miujiza. Allah(s.w) aliwapa mitume miujiza ili kuwa dalili ya kuwathibitishia watu kuwa yeye ndiye aliyewatuma. Hakuna Mtume au Nabii aliyedai kufanya miujiza kwa uwezo wake mwenyewe. Na hivi ndivyo Nabii Isa alivyowaambia wana wa Israili.
.........Nimekujieni na hoja kutoka kwa Mola wenu, ya kwamba nakuumbieni, katika udongo, kama sura ya ndege, kisha nampuliza, mara anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu na wenye mabalanga, na ninawafufua waliokufa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na nitakuambieni mtakavyo vila na mtakavyo weka akiba katika nyumba zenu. Bila shaka katika haya imo hoja (ya kuonesha kuwepo Mwenyezi Mungu) kwenu ikiwa ni watu wa kuamini(3:49)
Ni dhahiri kuwa miujiza yote aliyoifanya Nabii Isa(a.s), aliifanya kwa lengo la kuwathibitishia watu kuwa yeye ametumwa na Mwenyezi Mungu. Katika Biblia, Yesu alibainisha hili wazi kabla hajafanya muujiza wa kumfufua Lazaro:
Yesu akainua macho yake juu, akasema: Baba nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini ni kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kuwa ndiwe uliyenituma. Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake umefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake (Yohana 11:41-44)
Kwa kuzingatia maandiko haya, utabaini kuwa hawasemi kweli wale wanaodai kuwa Yesu ni Mungu eti kwasababu alifanya miujiza ya kufufua wafu.
Wito wa Nabii Isa(a.s) kwa Wanafunzi Wake
Nabii Isa(a.s) alipoona ukaidi wao umeshitadi, akatoa wito maalum kwa wanafunzi wake ili wajitokeze wale watakaokuwa tayari kuwa naye bega kwa bega kupambana na madhalimu na kuufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa wengine. Hivyo, akawauliza:
Lakini Isa alipoona ukaidi wao, alisema: Nani watakuwa wasaidizi wangu katika kumtangaza Mwenyezi Mungu (mmoja)? Wanafunzi wakasema: “Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemwamini Mwenyezi Mungu na ushuhudie kwamba sisi tumejisalimisha. Mola wetu! Tumeyaamini uliyoyateremsha na tumemfuata Mtume, basi tuandike pamoja na washuhudiao (3:52-53)
Baada ya hapo, wanafunzi wa Nabii Isa (a.s) wakamtaka awaombee chakula maalumu kutoka kwa Allah(s.w), wakasema:
Ewe Isa Mwana wa Maryam! Je Mola wako anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema(Nabii Isa), “Mcheni Mwenyezi Mungu kama kweli ninyi ni wenye kuamini kweli(5:112) Wakasema: “Tunataka kula katika hicho, na ili nyoyo zetu zitulie na tuwe miongoni mwa wanaoshuhudia(muujiza huo)(5:113) Akasema Isa bin Maryamu: “Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu! Tuteremshie chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu, na wa mwisho wetu, na kiwe Ishara itokayo kwako, basi turuzuku, kwani wewe ndiye mmbora wa wanaoruzuku(5:114)
Mwenyezi Mungu akasema: “Bila shaka Mimi nitakiteremsha juu yenu, lakini miongoni mwenu atakayekataa baada ya haya, basi Mimi nitamuadhibu adhabu ambayo sijamwadhibu yoyote katika walimwengu(5:115)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 web hosting 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Kuangamizwa kwa jeshi la tembo mwaka alizaliwa Mtume Muhammad s.a. w
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w sehemu ya 4. Hapa utajifunza kuhusu historia ya kuangamiza kwa jeshi la tembo.
Soma Zaidi...Mtume (s.a.w) alivyoandaa ummah wa kiislamu makkah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Vita vya Al Fijar na sababu zake
Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar.
Soma Zaidi...Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume
Uchaguzi wa ‘Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.
Soma Zaidi...MJADALA JUU YA NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA)
LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam).
Soma Zaidi...