Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah

Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Zoezi la 7.

  1. (a)    Nini maana ya ‘zama za Jahiliyyah’?

(b)  Bainisha baadhi ya mambo aliyoyakuta Mtume (s.a.w) katika jamii ya waarabu wa Makkah zama za Jahiliyyah.

  1. Mji wa Makkah ni mji mkongwe na mtukufu tangu zama za Nabii Ibrahim (a.s). Thibitisha kauli hii kwa kutoa sababu ya utukufu wa mji wa Makkah.
  2. (a)  Bainisha sababu zilizopelekea Muhammad (s.a.w) alipokuwa mdogo   kwenda kulelewa nje ya mji wa Makkah.
    1.     Taja baadhi ya sifa au tabia za Mtume (s.a.w) alizokuwa nazo tangu utotoni zilizokuwa kama ishara ya kuandaliwa kuwa Mtume wa Allah.

 

  1. (a)  Bainisha maandalizi ya Mtume (s.a.w) kabla ya kupewa Utume (mafunzo ya Ki-Ilhamu).

(b)  Ni yapi mafunzo yatokanayo na Maandalizi ya Mtume (s.a.w) ya Ki-Ilhamu?

  1. Mtume (s.a.w) alianza kupewa mafunzo ya Ki-wahyi mara tu baada ya kuanza kumshukia sura tatu za mwanzo, (96:1-5), (73:1-10) na (74:1-7).

    Kutokana na aya hizi ainisha mafunzo yatokanayo.

  1. (a)  Ni sababu zipi za msingi ziliwafanya Maquraish wa Makkah kuupinga Ujumbe wa Qur’an?
    1. Ainisha njia na mbinu walizotumia Maquraish katika kuupinga na kuuzuia ujumbe wa Uislamu kuenea katika jamii na mafunzo yatokanayo.

 

  1. Changanua njia alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuandaa ummah wa Kiislamu Makkah kwa kutumia mikataba ya ‘Aqabah.

 

  1. Katika kuendesha harakati za kuusimamisha Uislamu, hatuna budi kuwa na mikakati madhubuti. Kwa kurejea historia ya Mtume (s.a.w) onyesha jinsi alivyotumia stretejia madhubuti wakati wa kuhama kwenda Madinah.

 

  1. ‘Hijra katika Uislamu si sawa na Ukimbizi, bali na stretejia za kuunganisha nguvu ya kuusimamisha Uislamu’. 

Kwa kutumia Hijra ya Mtume (s.a.w), mambo gani waislamu wa leo tunajifunza katika hatua za kuupigania Uislamu. 

 

**********************************************

Wabillah Tawfiiq

**********************************



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/08/Saturday - 01:50:08 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1182


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 04
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SALIH(A.S
Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Waliomuamini Nabii Nuhu(a.s)
Waliomuamini Nuhu(a. Soma Zaidi...

Hali za bara arab zama za jahiliya karne ya 6 kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad
7. Soma Zaidi...

Kupotoshwa Mafundisho ya Nabii Isa(a.s)
Pamoja na Isa(a. Soma Zaidi...

Kujengwa upya al Kabah baada ya kuwa na mipasuko.
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 18. Hapa utajifunza kuhusu tukio la kujengwa upya kwa al kaaba ' Soma Zaidi...

Imam Abu Daud na Sunan Abi Daud
Soma Zaidi...

Vipengele vya mkataba wa Hudaibiya na faida zake katika Ukombozi (ufunguzi) wa mji wa Makkah
Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee 'Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Soma Zaidi...

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...

tarekh 01
NASABA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Kulingania Uislamu kwa Jamii Nzima
Baada ya miaka mitatu ya Utume, Muhammad(s. Soma Zaidi...