Vipi Allah huwasiliana na wanadamu kwa kupitia njia ya maandishi
Allah hutumia maandishi kuwafundisha wanadamu. Mfano mzuri ni nabii Musa ambaye alipewa vibao vya maandishi.
(e) Njia ya Maandishi: Njia nyingine anayoitumia Allah (s.w) katika kuwasiliana na waja wake ni njia ya maandishi, yaani maandishi yaliyoandikwa tayari. Nabii Mussa (a.s) aliletewa ujumbe kutoka kwa Allah (s.w) kwa maandishi yaliyoandikwa tayari katika mbao kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
“Na tukamwandikia katika mbao kila kitu mawaidha (ya kila namna) na maelezo ya kila jambo. Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu wako wayashike vema haya…” (7:145)
“Na Musa zilipotulia ghadhabu zake, aliziokota zile mbao. Na katika maandiko yake (hizo mbao) ulikuwamo uwongofu na rehema kwa wale wanaomuogopa Mola wao”. (7:154). Kwa ujumla tumeona kuwa chanzo cha elimu ni “Allah (s.w).
Lolote tunalolifahamu tumefunzwa na Allah kwa njia mojawapo katika njia tano tulizoziona.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Bongolite - Game zone - Play free game π2 Kitabu cha Afya π3 Kitau cha Fiqh π4 web hosting π5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π6 ai web app
Post zinazofanana:
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida
Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?
Soma Zaidi...Neema za Allah(s.w) Juu ya Bani Israil
Katika Qur'an tunakumbushwa neema mbali mbali walizotunukiwa Bani Israil (Mayahudi) na Mola wao ili kuwawezesha kusimamisha Ufalme wa Allah(s.
Soma Zaidi...