Ni ipi hasa siku ambayo nitafute ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kutafuta ujauzito
NI IPI HASA SIKU AMBAYO NITAFUTE UJAUZITO?
Kama ulipojifunza hapo juu kuwa zipo siku maalaumu ambazo yai hukomaa. Katika siku hizo mojawapo yai huletwa kwenye mirija ya falopia. Baada ya kukokotoa siku zako hapo juu sasa itakubidi kuongeza siku moja ama mbili nyuma. Hii ni kwa sababu makadirio ya siku hutofautiana. Na si lazima kkutafuta toto katika siku zote hizi. Unaweza kuruka kwa siku moja moja.
Jitahidi kufanya tendo la ndoa hasa katika siku hizo nne ulizozipata baada ya kukokotoa. Katika siku hizo jitahidi kufanya tendo siku ambayo itakuwa na sifa zifuatazo:-
1.Majimaji ya mwanamke ukeni yatakuwa ni mengi kuliko siku zilizopita. Mwanamke mwenyewe anaweza kujichunguza hali hii na kuigundua ila taabu. Anaweza kutumia kidole ama kitambaa safi kuchunguza uwepo wa majimaji haya katika ukeni kwake. Kumbuka hali hii isiambatane na shida nyingine za afya kama PID. Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuchunguza hasa kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa hasa kwa kutumia vidonge vya homoni.
2.Joto la mwanamke litakuwa ni kubwa kuliko siku nyingine. Joto hili sio homa, na lisiambatane na sababu nyingine kama maumivu ya kichwa, ama kutokana na kulala sana, ama misongo ya mawazo. Kikawaida siku ambayo yai hutolewa joto la mwanamke linakuwa kubwa hivyo akishiriki siku hii ujauzito ni rahisi kuingia.
3.Siku ambayo mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo. Wakato ambapo yai hutolewa kuna homoni huzalishwa kwa wingi. Homoni hizi zinaweza kusababisha mwanamke kutamani sana kushiriki tendo zaidi ya siku nyingine.
Pindi mwanamke atakapojigundua kuwa siku hii ameipata basi ni vyema kushiriki tendo ndani ya siku hii ama siku itakayofata haraka iwezekanavyo, maana yai la mwanamke linaweza kufa ndani ya muda mchach masaa 12 mpaka 24.
Kuna baadhi ya wanawake wanapata changamoto kutokana na kuwa na shida ya homoni katika mfumo wao wa uzazi. Hawa ni wale ambao siku zao hawazipati katika mpangilio sawa. Ni vyema wakafika kituo cha afya kupata matibabu ya tatizo hilo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
kunauwezekano wa darri ya kchefuchefu ictokee kabsa kwa mjauzito
Kichefuchefu ni moja katika dalili za mimba za mapema, Lucinda je upo uwezekano kwa mwanamke kuwa na ujauzito bila hata ya kuwa na kichefuchefu?
Soma Zaidi...Malengo kwa Akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba.
Posti hii inahusu zaidi malengo kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, ni malengo ambayo yametolewa ili kuweza kusaidia mtoto azaliwe vizuri na mambo mengine kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Magonjwa ya kwenye ovari na Dalili zake.
Post hii inahusu zaidi Magonjwa yanayoshambulia sana ovari na Dalili zake, haya ni magonjwa ambayo yanashambulia sana ovari ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu
Abali mkuu Nina mdogo wangu anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu na zenye kutisha uume wake nao umekuwa unakama mabaka umebabuka aisee nime angaika Sana kumtibia mpaka nakata tamaa
Soma Zaidi...Ndug mi naitaj ushauri mimi nishaingia kwenye tendo dakika 7 tu nakua nishafika kilelen naomba ushauri ndugu
Kama unadhani una tatizo la kuwahi kufika kileleni basi post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...