Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa uzazi wa mpango kwa watoto, sio akina Mama peke yao wanaofaidika na uzazi wa mpango vile vile na watoto wanafaidika na uzazi wa mpango kama ifuatavyo.
Faida za uzazi wa mpango kwa watoto.
1.kwanza kabisa tunajua lengo kuu la uzazi wa mpango ni kupata namba ya watoto wanaohitajika na kuwapa nafasi ya kutosha kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine, kwa hiyo na watoto wanapata faida ya uzazi wa mpango kama ifuatavyo.
2.uzazi wa mpango ukitumiwa ipasavyo unawapa watoto nafasi ya kupendwa na wazazi wao kwa mfano watoto wakizidiana miaka minne kwa vyovyote yule mtoto atainja mapenzi ya wazazi wake kuliko wale watoto wanaozidiana mwaka mmoja mmoja kwa hiyo tuwape watoto nafasi kati ya mtoto mmoja kwenda mwingine ili waweze kuonja mapenzi ya kweli kutoka kwa wazazi wao.
3.Pia uzazi wa mpango unawapa watoto nafasi ya kunyonya kwa mda mrefu , tunajua wazi kubwa mtoto alinyonya kwa mda unaofaa anakuwa na afya nzuri pia anaweza kukingwa dhidi ya magonjwa kuna wataalamu wanasema mtoto alkinyonya kwa mda wa kutosha anakuwa na akili za kufikiria kwa hiyo tuwape watoto mda waweze kunyonya kwa mda wa kutosha.
4.Uzazi wa mpango inawasaidia watoto wapate elimu ya kutosha kwa sababu mtoto akikaa na Wazazi kwa mda anajifunza mambo mengi kuliko wakiwa wengi na pia wazazi wataweza kupata Ela na kumpeleka mtoto wao shule nzuri kuliko kama wangekuwa wengi.
5.Pia uzazi wa mpango unasaidia kupunguza vifo vya watoto wakiwa wadogo , kwa sababu ya kukosa mahitaji muhimu au kuzaliwa wakiwa hawajafikishwa umri au na uzito mdogo kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa hata watoto wenyewe ikiwa wazazi wakitumia njia ya uzazi wa mpango nao wanapata faida kwa hiyo wazazi na jamii kwa ujumla mnaalikwa kutumia njia za uzazi wa mpango ili kuyafanya maisha ya watoto yapendeze
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu msaada kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi, hizi ni huduma ambazo utolewa kwa wale wenye maumivu ya tumbo la hedhi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi, kwa kawaida kondo la nyuma huwa nyuma ya mlango wa kizazi ila Kuna wakati kondo la nyuma ujishikisha mbele ya mlango wa kizazi.
Soma Zaidi...Jifunze sababu kuu zinazosababisha kuhisi maumivu makali ya tumbo wakati wa kushiriki tendo la ndoa
Soma Zaidi...Kuzaliwa kabla ya wakati humpa mtoto muda mdogo wa kukua tumboni. Watoto waliozaliwa kabla ya wakati, hasa wale waliozaliwa mapema, mara nyingi huwa na matatizo magumu ya matibabu.
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na huduma kwa mama wajawazito na waliojifungua.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tabia mbalimbali za Ute wa ovulation kwa sababu Ute huu huwa tofauti na Ute mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa tabia zake za kipekee kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Kunyonyesha ni moja katika njia za asili za kuzuia upatikanaji wa miba nyingine. Hata hivyo hii haimaanishi kuwa huwezi kupata mimba ukiwa unavyonyesha.
Soma Zaidi...