Madhara ya kaswende kwa wajawazito na watoto wadogo.

Posti inahusu zaidi madhara ya kaswende kwa mama mjamzito na mtoto, Ni ugonjwa unaopatikana hasa kwa njia ya kujamiiana na utoka kwa mwenye Ugonjwa kwenda kwa mtu ambaye hana ugonjwa, kwa hiyo tunapaswa kujua madhara ya ugonjwa huu kwa mama mjamzito na mt

Madhara ya kaswende kwa wajawazito na watoto

1. Kwanza tuanze kwa Mama, ugonjwa huu usababisha Mimba kutoka kwa sababu Maambukizi uingilia sehemu ambayo imefungwa kwa ajili ya kuzuia kitu chochote kupita na kushambulia sehemu mbalimbali kwa mtoto hatimaye mimba utoka kwa hiyo hali hii inasababisha maumivu makali kwa mama na wote waliomzunguka.

 

2. Kujifungua mtoto mfu.

Kwa sababu ya Ugonjwa wa kaswende mama anaweza kubeba mimba kwa miezi tisa lakini baadaye akajifungua mtoto mfu, kwa hiyo Mama mjamzito anapaswa kupima kaswende pale anapoanza tu mahudhurio ya kliniki na kuanza kutumia dawa mara moja.

 

3. Kuzaa mtoto kilema.

Ugonjwa huu wa kaswende usababisha sana kuzaliwa kwa watoto walemavu kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi ambayo ushambulia sehemu mbalimbali za mwili na kumfanya mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu na pia kuendelea kuwepo kwa ugonjwa huu umpata Mama kuingia kwenye risk ya kupata Maambukizi ya HIV na magonjwa mengine nyemelezi.

 

4. Pia na kwa mtoto mwenyewe kuna matokeo katika kuwa na ugonjwa huu ambapo ni pamoja na mtoto kuzaliwa akiwa na afya mbaya na kuwa na uzito mdogo ambapo wazazi utumia gharama na mda mwingi katika kumtibu mtoto, kwa hiyo mtoto akizaliwa tu anapaswa kupimwa kaswende kama hali yake sio nzuri kiafya na baba na Mama nao pia wanapaswa kupima ili kupewa madawa.

 

5. Jamii inapaswa kupewa elimu kuhusu ugonjwa huu, hasa wanawake wajawazito wanapaswa kuelezwa wazi na wahudumu wao au wauguzi kuhusu kupima na kupewa dawa ili kumkinga mtoto na hatari mbalimbali kama vile ulemavu wa viungo, kuzaliwa na kaswende na kuzaliwa mfu.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 3085

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Msaada kwa Mgonjwa aliyeshindwa kupitisha mkojo.

Posti hii utokea huduma ya kwanza kwa mtu aliye na shida ya kushindwa kupitisha mkojo kutoka kwenye kibofu Cha mkojo,

Soma Zaidi...
Dalili za tonsillitis (mafindo mafindo)

Tonsillitis kwa kiswahili hujulikana kama mafundomafundo ambayo hutokea pande mbili karibu na Koo na huwa na uvimbe na zikikaa kwa muda bila matibabu hutoa usaha.Dalili na dalili za ugonjwa wa tonsillitis ni pamoja na

Soma Zaidi...
Dalili za vidonda vya tumbo

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za vidonda vya tumbo

Soma Zaidi...
Bawasili usababishwa na nini?

Posti hii inahusu zaidi visababishi vya ugonjwa wa Bawasili,kuna watu wengi wanapenda kujua kabisa chanzo cha kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii na kuna maswali mengi yanayoulizwa kuhusu visababishi vya Bawasili.

Soma Zaidi...
Fahamu aina mbalimbali za Magonjwa nyemelezi ya moyo

Posti hii inahusu zaidi aina mbalimbali za Magonjwa ya moyo,kwa kawaida tunajua wazi kuwa kuna moyo mmoja lakini moyo huo unaweza kushambuliwa na magonjwa kwa kila aina kwa mfano kuna Maambukizi kwenye mishipa ya moyo,au kubadilika kwa mapigo ya moyo na m

Soma Zaidi...
Dalilili za saratani ya utumbo

Saratani ya Utumbo ni Saratani ya utumbo mpana (koloni), sehemu ya chini ya mfumo wako wa usagaji chakula. Kwa pamoja, mara nyingi hujulikana kama Saratani ya utumbo mpana. Visa vingi vya Saratani ya utumbo mpana huanza

Soma Zaidi...
MALARIA INATOKEAJE? (Namna ambavyo malaria inatokea, inaanza na inavyoathiri afya)

Kama tulivyokwisha kuona kuwa malaria inaweza kuambukizwa kwa kung'atwa na mbu aina ya anophelesi.

Soma Zaidi...