Funga za kafara

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

    -    Ni funga anazolazimika muislamu kufunga ili ziwe kitubio au fidia baada ya kutenda  kosa fulani.

 

  1.   Kufunga miezi miwili mfululizo kwa muislamu aliyemuua mtu kwa bahati mbaya na akakosa mali ya kulipa fidia.

Rejea Qur’an (4:92).

  1.   Kufunga miezi miwili mfululizo kwa muislamu aliyemsusa mkewe kwa kumfananisha na mama mzazi wake.

Rejea Qur’an (58:1-4).

 

  1.   Kufunga siku tatu mfululizo kama kafara kwa muislamu aliyevunja kiapo.

Rejea Qur’an (5:89).

 

  1.    Kufunga miezi miwili mfululizo kwa mume na mke waliofanya jimai (tendo la ndoa) mchana wa mwezi wa Ramadhani.

 

  1.    Kufunga kama kitubio cha muislamu aliyewinda na hali yuko katika Ihram.

-    Idadi ya siku inategemea na thamani ya kile alichokiua (alichokiwinda).

-    Kama hana uwezo wa kufunga, atatoa fidia ya mbuzi au kondoo.

      Rejea Qur’an (5:95).

 

  1.    Kufunga siku 10, tatu akiwa Makkah na 7 baada ya kurejea nyumbani kwa muislamu aliyevunja miiko ya Ihram.

-    Kama hana uwezo wa kufunga, atafidia kwa kuchinja mbuzi au kondoo.

Rejea Qur’an (2:196).

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2514

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana: