Malezi ya Mtoto Mchanga baada ya Talaka
Mtoto mchanga hataachanishwa na mama yake mpaka awe na umri wa miaka miwili - umri wa kuacha kunyonya. Matumizi ya mama na mtoto katika kipindi hiki cha kunyonya mtoto yatakuwa juu ya mume japo mkewe aliyemtaliki atakuwa kwa wazazi wake au penginepo nje ya nyumbani kwake. Lakini mume na mke walioachana, wakiridhiana wanaweza kumwachisha kunyonya kabla ya miaka miwili au wanaweza kumkodisha mwanamke mwingine amnyonyeshe. Hukumu hii ya malezi ya mtoto baada ya mume na mke kuachana inabainishwa vyema katika Qur-an:
Na wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili; kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha; na ni juu ya baba (yake) chakula chao (hao watoto na mama) na nguo zao kwa sheria. Wala haikalflshwi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya wasaa wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake, wala baba (asitiwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake).
Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa (kabla ya miaka miwili), kwa kuridhiana na kushauriana, basi sio kosa juu yao. Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha (wengine wasiokuwa mama zao) basi haitakuwa dhambi juu yenu kama mkitoa (kuwapa hao wanyonyeshaji) mlichowaahidi kwa sharia. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayoyatenda. (2:233)
Umeionaje Makala hii.. ?
Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ صَخْرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم يَقُولُ: "م...
Soma Zaidi...Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii.
Soma Zaidi...Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba?
Soma Zaidi...