Vita Kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali
Khabari za kutekwa Basra zilimchukua kwa mshangao mkubwa Khalifa Ali ambaye alikuwa aende Syria kumrudi Muawiya lakini alilazimika kwenda Basra kwanza kutuliza hali ya kule.
Alipofika Dhi-Qarโa mahali karibu na Basra-alituma ujumbe kwa Aisha, Talha na Zubeir wafanye mazungumzo ya amani. Nafasi ilipatikana mazungumzo yakafanywa na wakawa karibu kukubaliana baada ya Ali kuahidi kuwa atawaadhibu wauwaji wa Uthman Dola itakapokuwa na amani. Lakini mpango wa amani haukuwa na maslahi kwa lile kundi la Ibn Sabaa ambalo lilifanya sehemu ya jeshi la Ali.
Walinongโonezana kuwa Ali anataka kufikia makubaliano ya amani na ameahidi kuwaadhibu waliomuua Uthman. Kundi hili lilikuwa ndilo lililomuua Khalifa Uthman halikupendezwa na mpango huu, wakaunda hila iliyochochea kutokea vita. Mbinu mbili walizitumia. Kwanza walipeleka umbea Basra kuwa Ali akiingia Basra atawafanya watumwa wakazi wote na atawaua vijana wote. Kwa sababu hii watu wa Basra lazima wapigane.66 Ibn Sabaa na wachochezi wake usiku usiku walivamia jeshi la mama Aisha ambaye aliarifiwa na kwa namna hii vita vikaanza. Vita hivi vinajulikana kwa jina la Vita vya ngamia.
Vita vilikuwa vikali kwa vile ukubwa wa jeshi ulilingana. Baada ya mapigano makali na kuuawa Waislamu wapatao elfu kumi, Talha aliuwawa na , Zubair aliacha kupigana na akawa anaelekea Madina ndipo akauliwa njiani. Wakati wote wa vita mama Aisha alikuwa katika sehemu ya uwanja wa vita akiwa amepanda ngamia. Kuwepo kwake kulifanya mapigano yaendelee kwa kasi kubwa, bila kukoma, ndipo Ali alipoamuru ngamia wake akatwe miguu ya nyuma. Ngamia aliangukia miguu yake ya mbele na kwa heshima zote akatolewa mama Aisha ndani ya kikalio cha ngamia na vita vikaisha. Mama Aisha akasindikizwa Madinah na kaka yake Muhammad bin Abubakar.
Baada ya vita, Ali alizungumza na Waislamu katika msikiti wa Basra na Waislamu wakampa mkono wa utii. Alipoondoka alimuacha Abdallah bin Abbas kuwa Gavana wa Basra.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 797
Sponsored links
๐1 Kitabu cha Afya
๐2 Madrasa kiganjani
๐3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
๐4 kitabu cha Simulizi
๐5 Kitau cha Fiqh
๐6 Simulizi za Hadithi Audio
Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah
Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah. Soma Zaidi...
Kuingia Kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Soma Zaidi...
Hijra ya Mtume(s.a.w) Kwenda Madinah
Njama za Kumuua Mtume(s. Soma Zaidi...
Vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Ibrahiim(a.s) Aomba Kupata Kizazi Chema
Nabii Ibrahiim na mkewe Sarah walikaa mpaka wakawa wazee bila ya kupata mtoto. Soma Zaidi...
Mateso waliyoyapata waislamu wa mwanzo Maka, na orodha ya waislamu walioteswa vikali
Pili, Maquraish walimuendea Mtume(s. Soma Zaidi...
TAREKH, HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
1. Soma Zaidi...
Imam Muslim na Sahihul Mslim
Soma Zaidi...
Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a. Soma Zaidi...
Mafunzo ya sura zilizochaguliwa
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Katika Mji wa Taif
Baada tu ya Mtume(s. Soma Zaidi...
Hatua mbili kuu za kushuka kwa Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...