Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali.
7.Swalatudh-Dhuhaa
Swala ya Dhuhaa ni sunnah inayoswaliwa kati ya kipindi cha baada ya jua kupanda juu kiasi cha mita tatu hivi na kabla ya jua kufikia katikati. Lakini ni bora kuswali katikati ya kipindi hicho.
Swala hii inaswaliwa kwa rakaa mbili mbili hadi zitimie nane, lakini kwa uchache unaweza kuswali rakaa mbili tu na pia unaweza kuswali zaidi ya rakaa nane.
Umuhimu wa swala ya Dhuhaa uko wazi. Kipindi kati ya swala ya Alfajir na Dhuhuri ni kirefu sana kiasi kwamba mja anaweza kusahau kumkumbuka na kumtaja Allah (s.w). Kama tunavyofahamu kumkumbuka Allah (s.w) kila wakati ndio ngao pekee ya kumzuia mja na mambo maovu na machafu. Hivyo Swalatudh-Dhuhaa kwa mtu mwenye wasaa katika kipindi hicho cha harakati nyingi za kutafuta riziki, itampa msukumo mpya wa kumkumbuka na kumuabudu Allah ipasavyo.
Kutokana na hadith iliyopokelewa na Abu Daud na Ahmad, Buraidah (r.a) amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Katika mwili wa binaadam kuna viungo (joints) 360 na binaadam ni lazima akitolee sadaka kila kiungo kimoja”. Watu wakauliza:“Nani awezaye kufanya hivyo ewe Mjumbe wa Allah?”Mtume akawajibu: “Mtu anaweza kufanya hivyo kwa kuondosha kitu chenye madhara njiani. Na iwapo hatoweza, kufanya hivyo basi rakaa mbili za Dhuhaa zitamtosheleza ”.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Hii ni hutuba ya ndoa kwa ufupi, Imekusanya mambo ya msingi yanayohitajika katika hutuba ya ndoa
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukuelezea sifa za kuwa maamuma na taratibu za kumfuata imamu.
Soma Zaidi...Kuingizwa au Kutolewa EdaKatika sheria ya Kiislamu hapana suala Ia kuingizwa au kutolewa eda na Sheikh.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kuhusu swala ya sinnah ya tawba.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa
Soma Zaidi...