UWANJA WA TEKNOLOJIA

Sehemu ya tisa

.

                                 JIFUNZE MATUIZI YA OCR KATIKA SIMU YAKO
OCR nifupisho cha optical character recognition. Ni mchakato wa kubadilisha picha ya maandishi au maandishi yaliyoandikwa kwenye picha kuwa maandishi ya kawaida ambayo unaweza ukayahaisha kwengine kama kukopi.
Tokeo la picha la OCR
Yaani kwa mfano umetumiwa picha ambayo ina maandishi na unataka kuyakopi maandishi hayo ukayapest kwengine hivyo mfumo huu unatumia OCR. Kwa mfano katika picha hii hapa tunataka kuchukuwa hayo maneno ili tukayapest kwenye text za kawaida. Au kwa mfano umetumiwa picha iloandikwa ujumbe mzuuri na ukataka kumtumia mtu kwa text za kawaida hivyo hakuna haja ya kusumbuka kuiandika tena kwa vidole vyako hivyo tumia OCR ili uweze kuipest text yako. sasa hebu tuone jinsi ya kufanya mchakato huu...... nitaonesha kwa hatua namna ambavyo tutakavyoibadilisha picha hiyo hapo chini kuwa text za kawaida kwa kutumia simu zetu.


1. Kwa nza unatakiwa uwe na application ya kuweza kubadilisha picha ya maandishi kuwa maandishi. Twende play kisha ukadaunlod application iitwayo TEXT FAIRY (OCR SCANNER)
2. Ifunguwe kisha uchaguwe picha yako unayotaka kuikopi maneno yake angalia video hapo chini.
3. Ikisha aliza kuichakata picha yako itakuletea text utaweza kuzikopi au kuzitengezea PDF. Pia kuna kipengele cha kuchaguwa lunga kulingana na picha yako
Huduma hii pia inapatikana kwa kutumia kompyuta abapo unaweza kubadilisha hard copy zilizoskaniwa na kuzifanya ziwe soft copy.

         › WhatsApp ‹ Whatsapp