image

Njia rahisi ya kudownload video YouTube

Posti hii inakwenda kukuelekeza kuhusu njia rahisi ya kudownload video YouTube

NJIA RAHISI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE

Teknolojia ya mawasiliano ni muhimu katika kuhakikisha kuwa ulimwengu unafikika kama kijiji kimoja na hapa ndipo unapata maana halisi ya neno UTANDAWAZA yaani kwa lugha ya kimombo ni globalization. Kuweza kulifanikisha hili tunahitaji kuwa na teknolojia uliyo madhubuti na rafiki kwa watumiaji. Tunahitaji pia teknolojia kwa ajili ya kuburudika, na hapa ninazungumzia mtandao mkubwa duniani kwa kuonyesha video nao ni youtube.

 

 

 

Youtube ni kitengo katika kampuni itambulikayo kama google iliyo chini ya kampuni mama inayoitwa Alphabet. Youtube ni mtandao mkuu wa kurusha na kushiriki video. Hapa utaweza kupata fursa ya kushiriki video yako kwenye hadhara (public) ama na watu maalumu uwapendao. Video hii inaweza pia kuwa live yaani mubashara moja kwa moja

 

 

 

Changamoto inayowakumbwa watu wengi leo wanashindwa kudownload video za kwenye youtube. Usijali, katika makala hii nitakuletea njia rahisi na nyepesi ya kudownload video ya youtube. Baada ya kuidownload video hiyo unaweza kuweka kwenye flash, memori ana CD na kuitazama kwenye vifaa vyako vingine kama TV, SABUFA N.K

 

 

 

Zipo njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia kudownload video ya youtube zipo nyingine za kuzunguruka sana kama kutumia tubemate. Ama kutumia youtube go ambapo utawza kuangalia video ya bila ya kuhitaji intanet yaani offline. Nitazungumzia njia hizi kwa ufupi kisha nitakuletea njia iliyo rahisi zaidi katika hizo:-

 

 

 

1.tubemate ni muda mrefu toka watumiaji wa simu za smartphone waanze kulalamika kuwa wanahitaji kudownload video za youtube. Tubemate ikaja kwa lengo la kutatua tatizo hili. App hii haipatikani playstore kwa hiyo usalama wake ni mdogo kwa taarifa zako za siri.

 

 

 

tubemate Kwa kutumia tubemate unaweza kudownload video na ikabakia kwenye simu yako. Video hii pia unaweza kuihamisha kutoka kwenye simu yako na kuipeleka kwingine ukutakako. App hii utaidownload kwenye tovuti ya tubemate kisha utaruhusu kuinstall APK kutoka unknown source. Baada ya hapo unaweza kuingia youtube ukiwa kwenye App hii. Utachangua ama kutafuta video unayoitaka na utabofya kitufe cha kudownload. Video yako itakuwa tayari kwa kudownload na kuifadhiwa kwenye simu yako.

 

 

 

App hii pia ni maarufu sana kwa hiyo unaweza kuipata kwenye tovuti kama updown. Tubemate ni msaada mkubwa kwa watumiaji wa simu. Kwani unaweza pia kudownload video zaidi ya moja kwa wakati mmoja na kuchagua format uitakayo kama mp3, mp4, n.k

 

 

 

youtubego2.YOUTUBE GO hii ni App nyingine inayopatikana youtube go pia unaweza kuipata App hii playstore. App hii ni salama kama utaidownload kutoka playstore ama kwenye tovuti mama ya youtube go. hapo mwanzoni App hii haikuwa ikipatikana nchi zote, ilikuwa ikipatikana india na maeneo yenye mtandao hafifu usiofikia 3g.

 

 

 

Lengo hasa la App hii ya youtube go ni kuwezesha kuangalia video hata ukiwa na mtandao mdogo ama maeneo ambayo netweki inazumbua. Kwa kutumia unaweza kudownload video na kuzitazama kwenye kifaa chako ukiwa kwenye App ya youtube go. Unachotakiwa ni kuinstall App kutoka playstore google play store baada ya hapo unafungua App kisha unatafuta video unayoitaka, ukisha bofya kuitazama itakuja meseji kama unavyoona kwenye picha hapo juu.

 

 

 

Kama unataka kuitazama bila ya kudownload utachagua ubora kulingana na MB ukizo nazo kwa mfano vide ya hapo juu ina MB 48 ukiiangalia kwa ubora mkubwa na kwa ubora mdogo ni MB 6. Kama unataka kuidownload utabofya neno download. Baada ya hapo utaona sehemu imeandikwa Download hapo utaziona video zote ulizo download.

 

 

 

Utatazama video hizo bila ya kuhitaji intanet wala mb. Pia unaweza kushiriki na mwenzio ambaye ana App hii kwenye simu yake. Youtube go imekuwa ni msaada mkubwa kwa watu wanaoishi kwenye maeneo yemye mtandao mdogo.

 

 

 

3.https://www.y2mate.com/en4 hii ni njia nyingine na iliyo rahisi kuitumia. Kwa kupitia njia hii utaweza kuidownload video kwa usalama zaidi, kisha utaiweza kwenye kifaa chako. Video hii utaweza kuitazama kwa kutumia njia yeyote unayoitaka.

 

 

 

Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye tovuti ya youtube kisha unatafuta video unayoitaka. Baada ya hapo utakopi link ya video kama inavyoonyeshwa kwenye picha hapo chini. Ukitoka hapo utaingia kwenye tovuti ya y2mate hapo utapest link. Chini utaiona video yako na utaona batani za kudownload kama inavyoonyeshwa kwenye picha hapo chini.

 

1. HATUA YA KWANZA: INGIA YOUTUBE NA KISHA KOPI LINK YA VIDEO

hatua ya kwanza

 

2. HATUA YA PILI PEST LINK YAKO KWENYE TOVUTI YA Y2MATE, au bofya hapa kuingia

hatua ya pili

 

3. HATUA YA TATU CHAGUA FOMATI YA VIDEO YA KUDOWNLOAD

hatua ya tatu

 

4. HATUA YA NNE DOWNLOAD VIDEO YAKO KWA KUBOFYA BATANI ILIYOANDIKWA DOWNLOAD

download

 

Zipo njia nyingi tuu za kudownload video youtube kwa mfamo cyberspaceandtime hiini tovuti inayoonyesha video zilizopo youtube pamoja na kutoa chaguzi za kuweza kudownload video bila hata ya kutazama matangazo.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-09     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1960


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA NA MAWASILIANA
1. Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

Jinsi ya kufanya simu yako iwe fasta
Posti hii inakwenda kukuelekeza njia za kufanya simu yako iwe fasta Soma Zaidi...

MUDA WA KUCHAJI SIMU YAKO AMA MUDA WA KUCHAJI BETRI YAKO
Wwatu wengi wamekuwa wakijiuliza ni muda gani hasa inapasa kuchaji simu, je nisubiri mpaka chaji iishe kabisa, ama nichaji ikiwa na asilimia ngap? Soma Zaidi...

Kujaa kwa memory au hard disc
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vitu vya kufanya endapo memory au hard disk itajaa Soma Zaidi...

SIMU KUSUMBUWA MTANDAO NINI SABABU
Kuna mambo mengi sana ambayo yanachangia simu yako kutokuwa na mtandao mzuri yaani network kuwa ndogo. Soma Zaidi...

Nini maana na Trojan na ni zipi athari zake kwenye kompyuta ama simu
Soma Zaidi...

Chanzo
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Yanayoathiri betri yako
Somo hili linakwenda kukuletea mambo yanayo athiri betri lako Soma Zaidi...

EPUKA MALWARE (VIRUSI, WORM NA TROJAN UKIWA MTANDAONI)
Malware ni neno pana na watu wengi si wenye kulitumia. Soma Zaidi...

teknolojia
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...