Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano.
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Akaunti kuhakiwa inamaana kuna mtu amelogin kwenye akaunti yako bila ya ruhusa yako ama bila ya kumpatia neno la siri. Facebook imeweka njia kadhaa kuhakikisha kuwa akaunti za watu zipo salama muda wowote.
Two-factor authentication ni katika njia mujarabu ambazo facebook wameweka ili kulinda akaunti za watumiaji wake. Kwa kutumia njia hii hata kama mtu anaijuwa password yako (neno la siri) hataweza kuingia kwenye akaunti yako ya facebook mpaka awe na laini yako ambayo namba yeke umeisajili facebook.
Njia hii inaongeza tabaka lingine la usalama wa akaunti yako ya facebook. Baada ya kuingiza neno la siri kwenye akaunti yako ya facebook, facebook watakutumia code (namba sita) kwenye laini yako ulioisajili facebook. Namba hizo utaziingiza kwenye kibox na ndipo utaruhusiwa kuingia kwenye akaunti.
Kuanza kutumia njia hii ingia kwenye setting, kisha security and login kisha Two-Factor Authentication. Utatakiwa kuingiza namba ya simu na maelekezo machache yatafuata. Utalogout kisha utalogin tena ili kuthibitisha huduma kama ipo tayari.
Njia hii itasaidia sana kwa wale ambao tayari password zao kuna watu wanazifahamu. Hata kama mtu anaijua password TROJAN) yako katu hataweza kuingia kwenye akaunti yako mpaka awe na laini yako. Karibia mitandao mingi inatumia njia hii ikiwemo google, linkedin, github na mingine mingi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Teknolojia Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 585
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Kujaa kwa memory au hard disc
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vitu vya kufanya endapo memory au hard disk itajaa Soma Zaidi...
Maana ya legacy contact katika Facebook
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya legacy contact katika facebook Soma Zaidi...
Njia rahisi ya kudownload video YouTube
Posti hii inakwenda kukuelekeza kuhusu njia rahisi ya kudownload video YouTube Soma Zaidi...
Je nitumie simu yangu wakati inachaji?
Somo hili linakwenda kujibu swali la je nitumie simu yangu wakati inachaji Soma Zaidi...
Matatizo katika hard disk
Posti hii inakwenda kukupa baadhi ya matatizo katika hard disk Soma Zaidi...
Jinsi ya kufanya simu yako iwe fasta
Posti hii inakwenda kukuelekeza njia za kufanya simu yako iwe fasta Soma Zaidi...
Chanzo cha matatiza ya simu/kompyuta
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...
Njia za kujilinda na malware
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujilinda na malware Soma Zaidi...
Nini maana na Trojan na ni zipi athari zake kwenye kompyuta ama simu
Soma Zaidi...
Kurudisha mafaili na data zilizopotea
Posti hii inakwenda kukupa elimu ya kurudisha mafaili na data zilizopotea Soma Zaidi...
OCR
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...
Epuka malware (virus,work)ukiwa mtandaoni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuepuka malware ukiwa mtandaoni Soma Zaidi...