makala hii itakuelezea mambo makuu ambayo ni hatari kwa usalama wa betri ya kifaa chako
Kuna mengi tu yanayodaiwa eti yanamaliza chaji haraka katika betrii yako. Hapa nitakutajia mambo makuu mawili ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa kumaliza chaji yako.
1.Kucheza gemu. Gemu ni katika makuu ambayo yanaongoza katika kumaliza chaji ya betri yako kuliko mambo mengine.Gemu zimegawanyika katika makundi mengi tu inatagemea na vigezo vya kuzigawanya ila katika makundi hayo VIDEO GAME zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kumaliza chaji kwa haraka katika simu au kompyuta yako.
Kwa mfano GTA, CONFLICT DESERT STORM, CALL OF DUTY kwa kompyuta au DREAM SOCCER au GUNSHIP BATTLE kwa upande wa simu. Kwa ufupi video game huwa zinatumia HIGH GRAPHICS kiasi kwamba graphics engine zinahitaji chaji ya kutosha ili ziweze kufanya kazi husika.
Katika gemu hizi zipo online video game ambazo kwa namna nyingine ndio ambazo kwa kiasi kikibwa zaidi zinachangia kumaliza chaji kuliko zile za offline. Kwa mfano SHIP BATTLE hii ni katika online game ambazo zinatumia high graphics hivyo huhitaji kula chaji kwa wingi.
Kwa ufupi ni kuwa gemu ambazo hazihitaji uwezo mkubwa wa graphics huwa hazili chaji sana ukilinganisha na zile ambazo huhitaji uwezo mkubwa wa graphics. Pia video game zinakula chaji sana kuliko gemu ambazo si video game. Hali kadhalika online game huwa zinatumia kiwango kikubwa cha chaji kuluko offline game. Jambo la kuongeza hapa katika matumizi ya chaji pia chaji itatumika kwa wingi zaidi tu pale mwanga wa screen utakapokuwa umeongezwa zaidi yaan full brightness.
2. Internet. Hii huchukuwa nafasi katika mabo yanayoongoza katika kula chaji ila inategemea pia na matumizi ya internet. Kwani wakati mwingine unaweza ukawa unatumia internet lakini ukawa unatumia chaji kiasi kidogo kwa mfano intanet kwa kuperuzi habari bila ya kuangalia video ama mapicha au google ads.
Katika intanet kuangalia online video kama youtube huchangia kwa kiasi cha hali ya juu katika kumaliza chaji kuliko kuperusi habari. Pia kucheza gemu kwa kutumia intanet kwa mfano ONLINE GAME hizi huchangia kwa kiasi kikubwa katika kumaliza chaji ya betrii yako kwa haraka zaidi. Pia chaji itatumika zaidi kama mwanga wa screen utakapokuwa mkubwa full brightness.
Kwa kifupi haya mambo mawili huchangia kwa kiasi kikubwa kumaliza chaji ya betrii au simu yako kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko mambo mengine.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Teknolojia Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 452
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Kitau cha Fiqh
Njia rahisi ya kudownload video YouTube
Posti hii inakwenda kukuelekeza kuhusu njia rahisi ya kudownload video YouTube Soma Zaidi...
Sababu za simu kusumbua mtandao
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sabau za simu kusumbua mtandao Soma Zaidi...
TEKNOLOJIA NA MAWASILIANA
1. Soma Zaidi...
Matatizo katika hard disk
Posti hii inakwenda kukupa baadhi ya matatizo katika hard disk Soma Zaidi...
Kufungua program nyingi kwa wakati mmoja
Posti hii inakwenda kukuelekeza njia za kufungua program nyingi kwa wakati mmoja Soma Zaidi...
Muda wa kuchaji simu yako
Posti hii itakwenda kukujuza juu ya kuda mzuri wa kuchaji simu yako Soma Zaidi...
Jinsi ya kutuma sms ndefu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kutuma sms ndefu Soma Zaidi...
Epuka malware (virus,work)ukiwa mtandaoni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuepuka malware ukiwa mtandaoni Soma Zaidi...
Kipi kingine utafanya ukiwa Facebook
Somo hili linakwenda kukueleza Mambo mengne unayoweza kuyafanya ukiwa Facebook Soma Zaidi...
Kutuma sms ndefu
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...
Maana ya legacy contact katika Facebook
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya legacy contact katika facebook Soma Zaidi...
Matumizi ya OCR katika simu yako
Somo Hili linakuleteq mafunzo ya OCR katika simu yako Soma Zaidi...