yanayoathiri betri ya kifaa chako

makala hii itakuelezea mambo makuu ambayo ni hatari kwa usalama wa betri ya kifaa chako

yanayoathiri betri ya kifaa chako

YANAYOATHIRI BETRY YAKO:


Kuna mengi tu yanayodaiwa eti yanamaliza chaji haraka katika betrii yako. Hapa nitakutajia mambo makuu mawili ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa kumaliza chaji yako.

1.Kucheza gemu. Gemu ni katika makuu ambayo yanaongoza katika kumaliza chaji ya betri yako kuliko mambo mengine.Gemu zimegawanyika katika makundi mengi tu inatagemea na vigezo vya kuzigawanya ila katika makundi hayo VIDEO GAME zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kumaliza chaji kwa haraka katika simu au kompyuta yako.

Kwa mfano GTA, CONFLICT DESERT STORM, CALL OF DUTY kwa kompyuta au DREAM SOCCER au GUNSHIP BATTLE kwa upande wa simu. Kwa ufupi video game huwa zinatumia HIGH GRAPHICS kiasi kwamba graphics engine zinahitaji chaji ya kutosha ili ziweze kufanya kazi husika.Katika gemu hizi zipo online video game ambazo kwa namna nyingine ndio ambazo kwa kiasi kikibwa zaidi zinachangia kumaliza chaji kuliko zile za offline. Kwa mfano SHIP BATTLE hii ni katika online game ambazo zinatumia high graphics hivyo huhitaji kula chaji kwa wingi.

Kwa ufupi ni kuwa gemu ambazo hazihitaji uwezo mkubwa wa graphics huwa hazili chaji sana ukilinganisha na zile ambazo huhitaji uwezo mkubwa wa graphics. Pia video game zinakula chaji sana kuliko gemu ambazo si video game. Hali kadhalika online game huwa zinatumia kiwango kikubwa cha chaji kuluko offline game. Jambo la kuongeza hapa katika matumizi ya chaji pia chaji itatumika kwa wingi zaidi tu pale mwanga wa screen utakapokuwa umeongezwa zaidi yaan full brightness.

2. Internet. Hii huchukuwa nafasi katika mabo yanayoongoza katika kula chaji ila inategemea pia na matumizi ya internet. Kwani wakati mwingine unaweza ukawa unatumia internet lakini ukawa unatumia chaji kiasi kidogo kwa mfano intanet kwa kuperuzi habari bila ya kuangalia video ama mapicha au google ads.

Katika intanet kuangalia online video kama youtube huchangia kwa kiasi cha hali ya juu katika kumaliza chaji kuliko kuperusi habari. Pia kucheza gemu kwa kutumia intanet kwa mfano ONLINE GAME hizi huchangia kwa kiasi kikubwa katika kumaliza chaji ya betrii yako kwa haraka zaidi. Pia chaji itatumika zaidi kama mwanga wa screen utakapokuwa mkubwa full brightness.

Kwa kifupi haya mambo mawili huchangia kwa kiasi kikubwa kumaliza chaji ya betrii au simu yako kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko mambo mengine.                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 163


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

NAMNA YA KUFANYA KILA KITU KWA VITENDO KUTUMIA PICHA, VIDEO AMA SAUTI
Jifunze kufanya mambo mbalimbali kwa vitendo, kwa kutumia picha, sauti ama video Soma Zaidi...

ABOUT BONGOCLASS
learn English Vocabulary Soma Zaidi...

viumbe
MAAJABU YA VIUMBE 1. Soma Zaidi...

LEARN VOCABULARY
learn English Vocabulary Soma Zaidi...

Kushika mwenendo wa kati "Na ushike mwenendo wa kati'." (31:19)
Mwenendo wa kati ni mwenendo ulioepukana na kibri na majivuno kwa upande mmoja na ulioepukkana na udhalili na unyonge kwa upande mwingine. Soma Zaidi...

FORM FOUR ENGLISH PAST PAPERS
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Soma Zaidi...

TEST AND EXAMS (MAJARIBIO NA MITIHANI)
Tumia nafasi hii kujipima kwa maswali mbalimbali. Soma Zaidi...

Geography in our real life
Geography in our real life. Soma Zaidi...

STANDARD FOUR ENGLISH TEST 13
Soma Zaidi...

PARTS OF MICROSCOPE
MICROSCOPE Microscope this is an instrument used for viewing objects which are too small to be seen by our naked eyes. Soma Zaidi...