JE NITUMIE SIMU YANGU WAKATI INACHAJI???

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza swali hili. Pia kutokana na baadhi ya video vilizoeneaga wakati fulani kuwa mtu alilipuliwa na simu yake kwa sababu alitumia ikiwa INACHAJI.

 

Ukweli ni kwamba kutumia simu wakati inachaji hakuwezi kuifanya iripuke hata kidogo, napia hakuwezi kuuwa betri yako. Mainjinia wa vifaa vya umeme wanatueleza kuwa katika simu kuna kifaa ambacho kinaundwa kama simu umesha jaa na kuizuia isichaji tena, hivyo hakuna madhara ya kuchaji simu hata kwa masaa 10.

 

Jambo la kuzingatia ni joto la betri yako. Wakati unapotumia kifaa chako hakikisha joto la simu yako halipandi kuwa la juu sana. Kwani hili joto ni hatari sana kwa maisha ya betri yako.

 

Ni vyema kama unatumia simu yako aidha ikiwa chaji au haipo chaji pindi joto la betri yako likipanda uipumzishe. Pia hakuna madhara ya kuilaza simu yako kwenye chaji.