EPUKA MALWARE (VIRUSI, WORM NA  UKIWA MTANDAONI

Malware ni neno pana na watu wengi si wenye kulitumia. Malware hukusanya maana za virusi, trojan, spyware na worm. Watu wengi wamezoea kutumia neno virusi. Utasikia mtu anasema kuwa simu yake ina virusi. Kwahiyo virusi ni sehemu ndogo sana ya malware.

 

Mara nyingi virusi hawawezi kuharibu mafaili kwenye kifaa chako ila huathiri utendaji wa kazi wa kifaa chako. Virusi huweza kujizalisha wenyewe kwa wenyewe ndani ya kifaa chako. Worm wanaweza kutembea kutoka faili moja mpaka jingine. Kuna tofauti kubwa kati ya virusi, worm na trojan.

 

Malware ni program ama software ama code zinazoingizwa kwenye kifaa chako kama simu ama kompyuta, na kuunganisha kifaashako na mitandao ya watu au kuharibu taarifa (data) za kwenye kifaa chako. Malwarei huweza kuingia kwenye kifaa chako kwa kupitia:

 1. Waya wa USB
 2. Flash
 3. Ukiwa mtandaoni kwa kudownload mafaili, kufungua email (barua pepe)
 4. Bluetooth
 5. Kushea mafaili kwa njia nyinginezo.

 

Malware huondolewa kwenye kifaa chako kwa kutumia program za kuondoa malware zijulikanazo kama antivirus. Kuna program (software) nyingi ambazo zinaweza kufanya kazi hui ya kuondoa malware ikiwemo virusi. Program hizo ni pamoja na avast, kerspersky, avag, window defender na nyinginezo nyingi. Pia kwa watumiaji wa simu google playstore inafanya kazi hiyo bure kwa kuscan App zote ulizoziinstall.

 

Njia za kujilinda na malware

 1. Weka antivirus kwenye kifaa chako.
 2. Hakikisha unascan kifaa chako mara kwa mara
 3. Scan waya wa USB
 4. Kuwa makini unapotuckuwa mafaili kwa kutumia bluetooth ama njia nyingine. Vi vyema ukascan mafaili hayo
 5. Kuwa makini na kudownload kitu usichokijua, ama kufungua mafaili ama email usisozijua.
 6. Kuwa makini na matangazo yanayotaka uclick eitha upate zawadi ama bonasi
 7. Scan mafaili yote ulioyadownload.