picha

Kipi kingine utafanya ukiwa Facebook

Somo hili linakwenda kukueleza Mambo mengne unayoweza kuyafanya ukiwa Facebook

KIPI KINGINE UTAFANYA UKIWA FACEBOOK

Facebook ni mtandao wa kwanza wa kijamii (social media) unaotembelewa na watu wengi. Mitandao mingine ni kama twitter, linkedin, youtube, whatsApp, instagram na mingine mingi. Facebook imeanzishwa huko marekani, na imekuwa ikiongeza nguvu kila kukicha na kuboresha huduma zake zaidi kila siku. Leo facebook imekuwa ni kituo cha kufanya mengi zaidi ya mtumiaji wa kawaida anavyotambua. Katika makala hii nitakueleza matumizi mengine ya facebook ambayo watu wengi hawayajui.

 

Mtumiaji wa kawaida wa facebook amezoea kulogin na kuchat kwa sms, kushare picha, maoni, video na masimuliz, kupiga simu ya sauti yu ama video. Pia hutumika facebook kwa kuhifadhi taarifa binafsi pamoja na kuupdate wasifu wako. Hebu tuone baadhi ya matumizi mengine unayoweza kuyafanya ukiwa facebook

 

1. Kutangaza biashara na wasifu wako. Facebook ni njia ya haraka kwa anayetaka kutangaza wasifu wake, biashara yake ama kampuni. Ukiwa marafiki, na watu wengi wanaokufuata unaweza kuitumia nafasi hii kwa ajili ya kutangaza kile unachokitaka watu wakijue.

2. Unaweza kutumia facebook kama kituo cha kukupatia kipato. Wapo watu wengi leo wanajiingizia kipato kwa kutumia facebook, kwa mfano watu wanaomiliki kurasa za video wanaweka matangazo ya watu na kujiingizia kipato. Pia unaweza kutumia fursa hii ya facebook kutangaza biashara yako na kupata wateja. Sambamba na haya unaweza kujiingizia kipato kwa kutumia makala unazoandika kwenye ukurasa wako unaoumiliki.

3. Unaweza kufanya mikutano ya siri, watu maalumu ama ya hadhara, inaweza kuwa kwa kutumia video ama kwa sauti tu. Halikadhalika pia mikutano hii inaweza kuwa ya njia ya maandishi kama mkipenda pia.

4. Pia unaweza kucheza gemu ukiwa facebook. Huna haja ya kudownload gemu, ukiwa na simu ya smartphone

5. Kukusanya taarifa kuhusu mtu, watu, kikundi ama kampuni. Taarifa hizi zinaweza kuwa: namba ya simu, barua pepe (email), familia, sehemu, marafiki, vitu anavyopenda, mawazo yake kuhusu siasa, dini ama jamii, tabia yake na vitu anavyochukia. Pia unaweza kupata taarifa za mtu kuhusu vitabu anavyosoma, watu anaowafuata, video ama miziki anayotazama na kusikiliza, tarehe ya kuzaliwa na anapofanya kazi ama shule alizosoma, sambamba na kiwango cha elimu yake. Miongoni mwa taarifa hizi watu wengi wanadangaya ukweli wa mambo hususani majina na tarehe ya kuzaliwa.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Teknolojia Main: Post File: Download PDF Views 1471

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Tofauti ya Trojan na virusi

Posti hii inakwenda kukupa tofauti za trojani na virusi

Soma Zaidi...
JINSI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE

NJIA RAHISI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE Teknolojia ya mawasiliano ni muhimu katika kuhakikisha kuwa ulimwengu unafikika kama kijiji kimoja na hapa ndipo unapata maana halisi ya neno UTANDAWAZA yaani kwa lugha ya kimombo ni globalization.

Soma Zaidi...
EPUKA MALWARE (VIRUSI, WORM NA TROJAN UKIWA MTANDAONI)

Malware ni neno pana na watu wengi si wenye kulitumia.

Soma Zaidi...