Posti hii inahusu kiungulia kwa wanawake wajawazito na tiba yake, ni ugonjwa au hali inayowapata wajawazito walio wengi kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito.
Kiungulia na tiba zake kwa wajawazito.
1. Kwanza kabisa kiungulia uwapo wanawake wajawazito wakiwa kwenye wiki kuanzia ya thelathini mpaka arobaini,hali huu utokea kwa sababu progesterone homoni inalegeza cardiac sphincter za tumboni na kusababisha acid kurudi kwenye oesophagus na kusababisha kiungulia, kwa hiyo wajawazito walipatwa na hali kama hizi hawapaswi kuogopa au kuwa na wasiwasi wajue kuwa ni kitu cha kawaida utokea na uisha tu baada ya kujifungua. Na pia wauguzi wanapaswa kuwaambia wazi wajawazito ili watambue Dalili kama hizi wakati wa ujauzito.
2. Hili kupunguza hali hii ya kiungulia wanawake wenye mimba wanapaswa kuepuka kuinama kwa mda mrefu wakati wanapokuwa wanafanya kazi zao za kila siku, kwa hiyo wanapaswa kujua hali yao kwa hiyo ni vizuri kufanya kazi wakiwa wamesimama pindi wakisikia hali ya kiungulia au wanaweza kuwekewa kiti au meza wakati wa kufanya kazi kama vile kuosha vyote na kufua wakafanya wakiwa wamesimama na pia wote waliowazunguka wanapaswa kujua hali huu na kuwasaidia akina mama wajawazito ili waweze kufanya kazi zao bila kuinama.
3. Kama hali ya kiungulia imezidi sana wajawazito wanapaswa kula chakula kidogo kidogo kwa siku ili kuepuka hali ya kupata kiungulia kwa mfano anaweza kula saa mbili, saa nne, saa sita, saa nane, saa kumi, saa kumi na mbili na kuendelea mpaka mda wa kulala, kwa kufanya hivyo anaweza kuepuka kupata kiungulia mara kwa mara, nimesema hivyo kwa sababu kuna akina mama wajawazito wanaopata kiungulia cha hali ya juu sana kuliko wengine na pia watu wa karibu wanapaswa kujua hili na kuona kuwa ni hali ya kawaida na kuendelea kumjali Mama katika kupambana na hali yake ya mda mfupi tu.
4. Pia wanawake wajawazito wanapaswa kulala wakiwa na mito ya kutosha ili kuepuka kiungulia na pia wajawazito kama hawajalala na mito ya kutosha wanaweza kuteseka sana wakati wa usiku au mda wowote wa kupumzika kwa hiyo wauguzi na wataalam wengine wa afya wanapaswa kumweleza mama huduma hii ya kutumia mito ili kupunguza kuwepo kwa kiungulia na pia watu wa karibu wa Mama mjamzito wanapaswa kuhakikisha kuwa Mama anapata mito kadiri ya uhitaji.
5. Pia hali huu ya kiungulia ikizidi hata kama ni kawaida kwa wajawazito wanaweza kwenda hospitalini, kwa maana kuna dawa ambazo utibu ugonjwa huu dawa hizi ni kama vile anti acid na sawa nyingine kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya, kwa hiyo tunapaswa kuwaambia ukweli pale hali ikizidi wajawazito wanapaswa kwenda hospitalini kupata dawa za kuwatuliza hali zao.
6. Kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa wanawake wenye mimba Upata magonjwa madogo madogo kama kiungulia na wanapaswa kupata huduma za muhimu kwao kwa hiyo jamii inapaswa kuwaelewa na kuwahudumia kwa kadiri inavyowezekana na kuwa pamoja nao kwa sababu haya matatizo madogo kama kiungulia ni ya mda tu na Mama akijifungua yanapotea mara moja.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post yetu ya Leo inaenda kutufundisha kuhusiana na uvimbe wa korodani moja au ambayo kitaalamu huitwa EPIDIDYMITIS. EPIDIDYMITIS ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa kiume wa uzazi. Epididymis ni mrija (tube) uliyoko nyuma ya korodani ambayo mbegu za kiume
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la tezi koo, ni tatizo ambalo uwapata watu mbalimbali ambapo Usababisha koo kuvimba na mgonjwa huwa na maumivu mbalimbali na pengine mgonjwa upata kikohozi kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye koo.
Soma Zaidi...Posti hii itakwenda kuelezea mambo machache kuhusu ugonjwa wa kisukari
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu fangasi wa sehemu za Siri
Soma Zaidi...Saratani ya Koo inarejelea Vivimbe vya Saratani vinavyotokea kwenye koo lako (koromeo), sanduku la sauti (larynx) au tonsils.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi matibabu ya vidonda vya tumbo nyumbani, ni njia ya kawaida ya kujitibu vidonda vya tumbo kama tulivyoona.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea njia za kujilinda na kujikinga na UTI
Soma Zaidi...Post hii inaenda kuzungumzia zaidi kuhusiana na mimba zinazoharibika . mimba huweza kuaribika au kutoka anzia miezi 3 na kuendelea .
Soma Zaidi...Maumivu ya mgongo yanaweza kuwa ni dalili inayoonyesha tatizo fulani la kiafya ikiwemo magonjwa au majeraha.
Soma Zaidi...Magonjwa ya kuambukiza: Ni yale yanayoweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine au kutoka kwa wanyama kwenda kwa mtu Mlipuko tukio lililoenea la ugonjwa katika jamii kwa wakati fulani ambao huonekana kama kesi mpya kwa kiwango ambacho kinazi
Soma Zaidi...