Tatizo la kutanuka kwa tezi dume.

Posti hii inahusu zaidi tatizo la kutanuka kwa tezi dume, ni tatizo ambalo linawakumba wanaume wengi kwa wakati huu kwa sababu ya kuwepo kwa maaambukizi kwenye tezi ambayo Usababishwa na vitu mbalimbali kama tulivyoona.

Tatizo la kutanuka kwa tezi dume.

1.Kwanza kabisa lishe ikiwa ndogo inaweza kusababisha kutanuka kwa tezi dume kwa sababu mtu kama hana lishe ni rahisi kila Maambukizi ambayo yapo uweza kumpata 

 

2. Kuwepo kwa sumu hasa kwenye ogani za uzazi,

Pengine kwenye organi za uzazi panakuwepo na sumu ambayo Usababishwa na matumizi ya kemikali mbalimbali ambazo zinatumika wakati wa kujamiiana.

 

3. Unywaji wa pombe hasa zile kali na uvutaji wa sigara kupita kiasi .

Haya yote uingiliana na sehemu za tezi na kuleta Maambukizi hatimaye kutanuka kwa tezi dume.

 

4. Kutokuwepo usawa katika vichocheo vya mwili.

Kwa kuwa tunafahamu kwamba kwenye mwili kuna vichocheo ambavyo ufanya kazi mbalimbali vikiongezeka au kupungua Usababisha kutanuka kwa tezi dume , vichocheo hivyo ni progesterone na oestrogen homoni na vinginevyo kwa kitaalamu huitwa ( hormonal lmbalance).

 

5. Magonjwa ya zinaa.

Kuwepo kwa magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, kaswende na mengine mengi yanayoweza kusababisha kutanuka kwa tezi dume.

 

6. Upasuaji wa korodan.

Kwa wakati mwingine kama kuna upasuaji wowote kwenye korodani  na pale kama kuna kitu kimekosewa kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha kutanuka kwa tezi dume.

 

7.Pengine Ugonjwa unaweza kuwa kwenye familia.

Kwa wakati mwingine kunakuwepo ile hali ya kurithi unakuta familia nzima ina Ugonjwa huo kwa hiyo inawezekana kubwa ni Ugonjwa wa familia.

 

8.umri kama umeenda.

Tunajua kabisa kama umri umeenda kuna uwezekano wa kupata magonjwa kwa sababu ya kushuka kwa kinga ya mwili kwa hiyo ugonjwa huu pia unaweza kuwapa wazee pia Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/09/Wednesday - 09:49:28 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 807


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-