KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.
![]()
![]()
KULELEWA NA BABU YAKE:
Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Mzee huyu alimpenda sana mjukuu wake kuliko ambavyo alivyokuwa anawapenda watoto wake. Alikuwa katu hamuachi mjukuu wake akiwa peke yake. Mzee Abdul Al-Muttalib alikuwa akiwekewa godoro kwenye kivuli cha Al-kabah na watoto wake wanakaa pembeni ya godoro kwa heshima ya baba yao, basi alikuwa Mtume (s.a.w) anakaa kwenye godoro lile. Baba zake wadogo wanapomtoa mzee Abdul al-Muttalib alikuwa akiwakataza na kuwaambia kuwa kijana huyu atakujakuwa na nafasi nzuri.
Mzee Abdul al-Muttalib alikuwa sikuzote akipendezwa na vitendo vya mjukuu wake. Mzee huyu aliendelea kumlea yatima huyu mpaka alipofikia umri wa miaka nane, na hapa ndipo mzee huyu alipofariki dunia na kuongeza majonzi zaidi kwa kijana huyu. Mzee Abdul al-Muttalib alifariki wakati Mtume (s.a.w) alipokuwa na umri wa miaka nane na miezi miwili na siku kumi (10).
Umeionaje Makala hii.. ?
Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.
Soma Zaidi...Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake.
Soma Zaidi...Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...Pamoja na Ucha-Mungu aliokuwa nao Nabii Sulaiman watu hawakuacha kumsingizia mambo machafu.
Soma Zaidi...“Na (kumbukeni habari hii) Mola wake alipomfanyia mtihani (Nabii) Ibrahiim kwa amri nyingi; naye akazitimiza.
Soma Zaidi...