Tamko la Wapatanishi
Baada ya mazungumzo marefu wapatanishi walikubaliana kuwa wote wawili Ali na Muawiyah hawafai kugombea nafasi ya ukhalifa. Amr bin al- As alimtegea Abu Mussa aanze yeye kusema msikitini juu ya maazimio yao. Abu Muusa akasema; “Enyi watu tumelizingatia vyema suala linalotukabili. Hatukuona njia nyingine ya kuleta amani miongoni mwa watu ila kuwaondoa wote katika nafasi ya kugombea Ukhalifa. Baada ya hivi mchague Khalifa anayefaa. Hii ndio hukumu yangu.
Alipopanda jukwaani Amr bin al As alibadili maneno na kusema maneno wasiyokubaliana na mwenziwe kwa kusema; “Mmesikia hukumu ya Abu Mussa. Amemuondoa mtu wake nami pia ninamuondoa. Lakini kwa chifu wangu Muawiyah, yeye ninamthibitisha, ni mrithi wa Uthman, mlipiza wa damu yake, ni bora kuliko wote kwa kuchukua nafasi yake.
Wajumbe wote walichanganyikiwa kwa kauli hii na kukawa hakuna maelewano. Nusra Amr bin al-As auliwe na askari wa Ali. Uamuzi huu haukufuata Qur’an hivyo haukukubalika. Khawarij walijikusanya na kuanza uasi. Walihama Harorah na kwenda Nahruwan. Katika eneo hili waliuwa watu na kufanya ukatili. Khalifa Ali alizungumza na Khawarij hawa ili waache vitendo vyao na imani yao potofu.
Lakini hawakukubali, kwa hali hii mapigano yakawa lazima, hata hivyo walishindwa vibaya. Baada ya hapa Khalifa Ali aliamuru jeshi lake liende Syria kupambana na Amir Muawiya kwa sababu suluhu haikuwa katika Qur’an. Lakini kabla ya kwenda Syria Khalifa Ali alipiga kambi mahali paitwapo Nakhila karibu na mji wa Kufa. Askari wake waliomba kwenda makwao na akawaruhusu, wengi hawakurudi na safari ikavunjika. Alijaribu mara mbili kukusanya askari kwenda Syria bila mafanikio na kutokana na hali hii suala zima la kupigana tena na Muawiya akaliacha.
Umeionaje Makala hii.. ?
Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a.
Soma Zaidi...Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w sehemu ya 4. Hapa utajifunza kuhusu historia ya kuangamiza kwa jeshi la tembo.
Soma Zaidi...Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua.
Soma Zaidi...KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Jitihada alizozifanya Khalifa wa Tatu katika kuilinda Quran
Soma Zaidi...