KULELEWA NA MAMA YAKE ALIPOFIKA MIAKA MINNE
Mtume (s.a.w) alirudishwa kwa mama yake alipokuwa na umri wa miaka minne, na aliendelea kuishi na mama yake mpaka alipotimia miaka sita, na hapo ndipo wakati ambao mama yake kipenzi alifariki dunia. Wanazuoni wanaeleza juu ya kufariki kwa mama yake kama ifuatavyo:-

Mama yake Mtume (s.a.w) alifunga msafara kwenda kuzuu kaburi la mume wake huko madina. Katika msafara huu alikuwepo Mtume (s.a.w), mjakazi wa kike aitwaye Ummu Ayman, Mtume (s.a.w) pamoja na baba mkwe wake bi Amina aitwaye ‘Abdul Al-Muttalib. Walikaa huko kwa muda wa mwezi mmoja, na walipokuwa wanarejea mama yake Mtume (s.a.w) alipatwa na maradhi ya ghafla na akafariki wakiwa njiani sehemu iitwayo Abwai ni kijiji kilichopo kati ya Makkah na madinah.